Na Kulwa Mzee, Dar es Salaam
ALIYEKUWA mgombea urais visiwani Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu wa
mwaka jana kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif
Hamad, leo amewasili Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kuwashtaki
viongozi anaodai wanaminya demokrasia visiwani humo.
Taarifa za Maalim Seif ambaye ni Katibu Mkuu wa chama hicho kuwasili
katika mahakama hiyo mjini The Hegue, zilibainishwa mjini Dar es Salaam
jana na Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Zanzibar), Nassor Mazrui
alipozungumza na waandishi wa habari.
“Maalim Seif alipeleka maombi Mahakama ya ICC, kajibiwa ndiyo maana
kesho (leo) anafika mahakamani kuelezea jinsi demokrasia inavyominywa
Zanzibar.
“Amepeleka vielelezo vingi, vikiwamo vya uvunjaji wa haki za
binadamu, baada ya maelezo mawakili wataendelea na utaratibu wa
kimahakama,”alisema Mazrui.
Katika uchaguzi wa marudio uliofanyika Machi 20, mwaka huu, baada ya
ule wa mwaka jana kufutwa, Maalim Seif hakushiriki kwa madai kuwa
haukuwa halali.
Alisema katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana uliofutwa na Mwenyekiti wa
Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salum Jecha, kwa madai kulikuwa
na kasoro nyingi, licha ya waangalizi wa kimataifa kusema ulikuwa huru
na haki.
Katika uchaguzi wa marudio, mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk.
Ali Mohamed Shein aliibuka mshindi kwa kupata kura 299,982 ambazo ni
sawa na asilimia 91.4, akifuatiwa na na mgombea wa Chama cha ADC, Hamad
Rashid Mohamed aliyepata kura 9,734 ambazo ni sawa na asiilimia 3.
IGP
Kuhusu kauli ya Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Ernest Mangu kuwa
jeshi hilo litamkamata na kumfikisha mahakamani Maalim Seif, Mazrui
alisema ni jambo ambalo haliwezekani.
Alisema hofu ya IGP Mangu, inatokana na kuona kuna kila dalili za
viongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) na yeye mwenyewe
kufikishwa mahakamani.
“Tunasema azma ya kuwafikisha mahakamani vinara wote wa uminyaji wa demokrasia na uvunjaji wa haki za binadamu iko pale pale.
“Ameamua kutumia mkakati wa kutaka kumkamata kiongozi kama njia ya
kujipapatua ili kuhakikisha lengo la CUF halifanikiwi,”alisema.
Alisema hakuna asiyejua Maalim Seif ni kipenzi cha Wazanzibari na ndiye anayeshinda uchaguzi mkuu wote Zanzibar.
Alisema jaribio lolote la kumkamata na kumdhalilisha kwa kumweka
ndani ni kulazimisha au kutaka kuitumbukiza Zanzibar na Tanzania katika
machafuko ambayo kiongozi huyo hapendi kuona yanatokea.
“CUF inamtaka IGP Mangu kufahamu, Maalim Seif na viongozi wote
hawatatishwa wala kurudishwa nyuma au kunyamazishwa kwa aina yoyote ya
vitisho katika kudai haki ya ushindi Zanzibar kutokana na uamuzi
uliofanywa Oktoba 25, mwaka jana,”alisema.
Alisema mpango wa kuishawishi dunia kuwachukulia hatua wahusika wote
wa ukiukwaji wa haki za binadamu na uminywaji wa demokrasia uko pale
pale hautasitishwa kwa vitisho.
“Kama vitisho vikiendelea, CUF tutakwenda kumtembelea IGP Mangu ofisini kwake,”alisema.
Alisema wanashangazwa kuona mpaka sasa IGP Mangu,ameshindwa
kumchukulia hatua za kumwajibisha Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) na
Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka ya Jinai (DDCI), Salum Msangi dhidi ya
kauli za vitisho na kibabe alizotoa kuhusiana na mawakili wanaofika
vituo vya polisi kuwawakilisha na kuwatetea wananchi waliokamatwa kwa
tuhuma mbalimbali.
Mwishoni mwa Juni, mwaka huu wabunge wa Ukawa walimtaka Rais Dk. John
Magufuli kutoa tamko juu ya uvunjifu wa haki za binadamu Zanzibar na
kwamba wana mpango wa kumpeleka Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC),
wakidai yanayotokea visiwani humo yana baraka zake.
Wabunge hao walimtaka pia Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba kwenda Zanzibar kujionea hali halisi badala ya kupata taarifa kutoka kwa wasaidizi wake.
Wabunge hao walimtaka pia Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba kwenda Zanzibar kujionea hali halisi badala ya kupata taarifa kutoka kwa wasaidizi wake.
Mwenyekiti mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), James
Mbatia alisema hali ya kiusalama inazidi kuwa mbaya Pemba na Unguja
kutokana na baadhi ya wananchi kupigwa na vikosi alivyodai ni vya
usalama.
MNYIKA
Wakati huo huo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na Katibu Mkuu wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC), Dk. Liberat Mfumukeko,wamefunguliwa
kesi ya kikatiba katika Mahakama ya Afrika Mashariki .
Kesi hiyo, imefunguliwa jana ambapo mlalamikaji wa kwanza, ni
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman
Mbowe,Mbunge wa Kibamba, John Mnyika na mlalamikaji wa tatu akiwa ni
Chama cha Chadema.
Akizungumza na waandishi wa habari, baada ya kufungua kesi
hiyo,Wakili wa Chadema, John Mallya alisema kesi hiyo ya kikatiba ni ya
kupinga uvunjifu wa vifungu vya mkataba ulioanzisha Jumuiya hiyo.
Alisema mkataba huo, unataka nchi ambazo ni wajumbe wa jumuiya hiyo
kuheshimu masuala ya kidemokrasia,vyama vingi na uhuru wa watu
kukusanyika.
“Nimeagizwa na wateja wangu Mbowe, Mnyika na Chadema,kuwafungulia
kesi na nimeshaiwasilisha mahakamani na tuna imani itapangiwa majaji na
hivi karibuni itaanza kusikilizwa”alisema na kuongeza
“Sababu za msingi za kufungua kesi hii, ni zuio ambalo polisi
wameliweka na Rais Magufuli amekuwa akilirudia mara kwa mara kwamba
vyama vya siasa havipaswi kufanya shughuli za siasa wakati huu hasa
mikutano ya hadhara hadi mwaka 2020,” alisema.
Kwa upande wake, Mnyika ambaye ni mlalamikaji wa pili katika kesi
hiyo, alisema Katiba ya Tanzania na Sheria zingekuwa zinaruhusu Rais
aliyeko madarakani kushitakiwa, kesi hiyo wangemshtaki Rais Magufuli
moja kwa moja.
“Sheri zetu zingekuwa zinaruhusu kumshitaki Rais,leo tungemburuza
Magufuli moja kwa moja, tutasimamia hoja mahakamani na tumeleta
vielelezo mbalimbali, ikiwemo barua ya zuio la Polisi,mikutano ambayo
imezuiwa ikiwamo wa Kahama…tunaamini vitakuwa ushahidi wa namna ambavyo
Serikali ya Tanzania kupitia Polisi kukiuka mkataba wa Jumuiya
Chanzo Na Mwananchi
0 comments:
Post a Comment