Emmanuel T. Kaaya
KUIMARIKA kwa Sekta ya Utalii katika ukanda wa Pwani ya Visiwa vya Zanzibar kumeanza kuleta athari kubwa ikiwemo kuzorota kwa shunguli za elimu kwa wanafunzi na utoro. Kijiji cha Michamvi kilichopo Wilaya ya Kusini Unguja kimeathirika na maendeleo ya Sekta ya Utalii baada ya wanafunzi wake wengi kuacha shule na kujishungulisha na kazi za kutembeza watalii.
Mkuu wa Kijiji cha Michamvi, Said Mlenge alithibitisha kuibuka kwa tatizo hilo ambalo limefanya mahudhurio ya wanafunzi wa Shule ya Michamvi kuzorota kwa kiasi kikubwa. “Tumepokea malalamiko kutoka kwa walimu wa Shule ya Michamvi kuhusu kuongezeka kwa utoro wa wanafunzi ambao hujishungulisha na kazi za kutembeza watalii katika maeneo ya fukwe na kuwapeleka baharini kuangalia rasilimali za baharini na samaki,” alisema Mlenge.
Afisa wa Elimu Mkoa wa Kusini Unguja, Ali Muhsin alikiri kupokea kwa malalamiko kutoka kwa Kamati ya Wazazi katika Kijiji cha Michamvi kuhusu mahudhurio mabaya ya wanafunzi ambao hujishungulisha na kazi za kutembeza watalii.
“Tumepokea taarifa na malalamiko ya wazazi Mkoa wa Kusini kuhusu mahudhurio mabaya ya wanafunzi katika shule hiyo ambao wamejishungulisha na kazi za Sekta ya Utalii,” alisema. Kijiji cha Michamvi Mkoa wa Kusini Unguja zipo zaidi ya hoteli 15 za kitalii ambazo zimetoa ajira zaidi ya 200 huku wavuvi wa kijiji hicho wakiuza samaki wao katika hoteli hizo kwa bei nzuri.

Chanzo: Jaridaletu
0 comments:
Post a Comment