TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUTOKA IKULU, ZANZIBAR

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ameipongeza Kampuni ya ‘Kunshan Asia Aroma Cooperation Limited” kutoka nchini China kwa uamuzi wake wa kuja kuekeza hapa Zanzibar.

Dk. Shein aliyasema hayo leo Ikulu mjini Zanzibar wakati alipokuwa na mazungumzo na ujumbe kutoka Kampuni ya “Kunshan Asia Aroma Cooperation Limited” kutoka nchini China ambayo imedhamiria kuekeza katika kiwanda cha Makonyo, kilichopo Wawi Pemba kwa kushirikiana na Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC).

Katika mazungumzo hayo, Dk. Shein aliihakikishia Kampuni hiyo kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itatoa ushirikiano wake mkubwa kupitia Wizara yake ya Biashara na Viwanda pamoja na Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC).

Dk. Shein alitumia fursa hiyo kuipongeza Kampuni ya “Kunshan Asia Aroma Cooperation Limited” chini ya Mwenyekiti wake Zhou Junxue kwa kusaini Makubaliano ya Awali kati ya Kampuni hiyo na Shirika la (ZSTC).

Aidha, Dk. Shein aliueleza ujumbe wa Kampuni hiyo kuwa Kiwanda cha Makonyo kilichopo Wawi ni cha muda mrefu ambacho kimekuwa kikizalisha mafuta ya aina mbali mbali hivyo, ushirikiano wa pamoja katika uzalishaji kiwandani hapo kutasaidia kuinua ubora wa kiwanda sambamba na kuongeza pato la Taifa na soko la ajira.

Alieleza kuwa uwamuzi wa Kampuni hiyo ni mzuri na umekuja katika wakati muwafaka ambapo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imo katika kutekeleza Sera ya Uchumi wa Viwanda, hivyo hatua hiyo itakuwa chachu katika kufikia malengo yaliyowekwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Pamoja na hayo, Dk. Shein alieleza kuwa Zanzibar imejaaliwa kuwa na viungo vya vyakula vya aina nyingi ambavyo miongoni mwao vimekuwa vikitoa mafuta bora ambayo yamekuwa ni bidhaa muhimu iliyoingia katika soko la ndani na nje ya Tanzania yakiwemo mafuta ya makonyo, mafuta ya karafuu na  mafuta ya mikaratusi.

Hivyo, Dk. Shein aliongeza kuwa kuanza kwa uwekezaji huo kutazidi kuitangaza Zanzibar na kuwa kiwanda cha pekee katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kinachozalisha bidhaa hizo za mafuta.

Sambamba na hayo, Rais Dk. Shein alieleza haja ya Kampuni hiyo kushirikiana na ZSTC katika kutekeleza makubaliano hayo yaliotiwa saini hapo jana ikiwa ni pamoja na kuongeza zaidi uzalishaji huku akisisitiza suala zima la ufanyaji utafiti katika kilimo cha mazao hayo yanazotoa mafuta.

Aidha, Dk. Shein alisisitiza suala la mafunzo ambalo litasaidia sana kuendesha kiwanda hicho pamoja na kuongeza uzalishaji wa bidhaa za aina mbali mbali za mafuta ya viungo kutoka katika kiwanda hicho cha Makonyo Wawi jambo ambalo pia, litaongeza soko la ajira hapa nchini.

Nae Mwenyekiti wa Kampuni ya “Kunshan Asia Aroma Cooperation Limited” ya China, Zhou Junxue alimpongeza Rais Dk. Shein kwa juhudi zake katika kuimarisha uchumi wa Zanzibar kwa kupitia sekta ya viwanda vikiwemo viwanda vidogo na vya kati.

Mwenyekiti wa Kampuni ya “Kunshan Asia Aroma Cooperation Limited” alimueleza Rais Dk. Shein mikakati iliyowekwa na Kampuni yake katika kuhakikisha makubaliano waliyosaini yanatekelezwa kwa lengo la kuleta manufaa kwa pande zote mbili.

Junxue alimuhakikishia Rais Dk. Shein kuwa Kampuni yake itatoa mashirikiano makubwa kwa Serikali kupitia Shirika lake la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC) katika kuhakikisha kiwanda hicho kinatoa mafuta yalio bora sambamba na kuongeza uzalishaji wa bidhaa zitakazozalishwa katika kiwanda hicho cha Wawi.

Kampuni ya “Kunshan Asia Aroma Cooperation Limited” ya nchini China ambayo ndio mnunuzi mkubwa wa mafuta ya viungo vya Zanzibar tokea Julai mwaka 2017, ilitiliana saini Makubaliano ya Awali na Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC) katika kuendesha mradi ndani ya miaka kumi utaohusisha uimarishaji wa utendaji na utaalamu katika kiwanda cha Makonyo Wawi.

Jambo jengine ni uendelezaji wa mazao ya karafuu na mikaratusi ili kuongeza uzalishaji kutoka tani 60 zinazozalishwa hivi sasa hadi kufikia tani 2,000,
ubadilishanaji uzoefu kati ya watendaji wa taasisi hizo, upatikanaji wa mafunzo, mbinu na upatikanaji  mbegu bora za mikaratusi ni miongoni mwa makubaliano hayo.
Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
 

MAKAMU WA RAIS AKISHIRIKI UJENZI WA SEKONDARI MICHEWENI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki ujenzi wa skuli ya Sekondari Micheweni mkoa wa Kaskazini Pemba. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Mwonekano wa ujenzi wa skuli ya Sekondari Micheweni mkoa wa Kaskazini Pemba

NDEGE YAANGUKA NA KUWAKA MOTO UWANJA WA NDEGE WA ZANZIBAR

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Marubani wawili wamefariki Dunia katika ajali ya ndege wakati wa kurusha ndege baada ya matengezo katika Uwanja wa Ndege wa Abeid Amani karume.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotekea jana majira ya saa saba Mchana Uwanjani hapo, Muhandisi Mkuu kutoka kampuni ya Tropical Air, David Kisusi  amesema ndege hiyo imeanguka na kuungua na kusababisha vifo kwa marubani hao ambao walikuwa ndani ya ndege hiyo.
Amesema ndege hiyo yenye usajili wa 5H-TDF yenye uwezo wa kubeba abiria wanne ni mali ya Chuo cha Usafirishaji cha Dar-es-Salam (NIT) ambayo ilikuwepo Zanzibar kwa ajili ya matengenezo.

Amesema takriban miezi sita ndege hiyo ipo hapa Zanzibar kwa ajili ya kufanyiwa matengenezo ili iweze kutumika katika chuo cha Usafirishaji .
Daktari Bingwa wa Uchunguzi katika Hospital ya Kuu ya Mnazi mmoja, Msafiri Marijani amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo na amesema vifo hivyo vimesababishwa na kukosa hewa safi wakati wa ajali hiyo pamoja na kathirika na moto uliotokea wakati wa kuanguka ndege hiyo.

Amesema uchunguzi ulifanywa katika miili ya maiti hao mnamo majira ya saa 12:45 jioni pia ulitokana na kukosa msaada wa kwa muda mrefu tangu ndege hiyo ianguke na kulipuka.
Wakati huohuo Mkuu wa Chuo cha Usafirishaji wa Anga kutoka Dar es Salaam, Dkt. Bwire Rufunjo alifika Zanzibar kwa ajili ya kufuatilia taarifa za ajali hiyo na amesema wamepokea taarifa hiyo kwa mshtuko mkubwa kutokana na vifo vya wafanyakazi hao muhimu katika sekta ya anga.

Aliwataja  marehemu kuwa ni Injinia Edger Alfred Mecha mwenye Umri wa miaka 26 na mwengine ni Dominic Bomani mwenye umri wa miaka 64 ambao walikuwa wanafanya kazi katika chuo hicho kwa ufanisi mkubwa.

Aidha amewataka wanafamilia wa Marehemu hao kuwa wavumilivu katika kipindi hichi kigumu kufuatia msiba huo pamoja na kutoa wito kwa wanafunzi wa chuo hicho kutokata tamaa wakati wa masomo.

Akizungumzia sababu ya kuanguka kwa ndege hiyo ndogo, amesema uchunguzi bado unaendelea lakini katika uchunguzi wa awali wamebaini kuwa ni hitilafu ya mfumo wa umeme ambao umesababishwa na moto ulilipuka kutokana na ndege kuwa na Mafuta mengi.

Ndege hiyo imenunuliwa kutoka kampuni ya Tropical Air ya Zanzibar kwa ajili ya kufundishia Urubani katika  Chuo cha Usafirishaji lakini kutokana na kutokuwa na hali Nzuri ililazimika kufanyiwa matengenezo na kampuni hiyo kabla kuchukuliwa na chuo.

Rais Shein Ahudhuria Chakula cha Mchana na Vijana wa Halaiki

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, wakijumuika na Vijana na Wanafunzi walioshiriki katika Halaiki ya kuadhimisha Miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar
BAADHI ya Wanafunzi na Vijana walioshiriki katika sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar, wakijumuika katika hafla ya chakula cha mchana kilichoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,kilichofanyika katika viwanja vya Vikosi vya KVZ Mtoni Zanzibar
BAADHI ya Vijana na Wanafunzi walioshiriki katika sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika viwanja vya Amaan Zanzibar
BAADHI ya Viongozi wa Halaiki wakiwa katika viwanja vya Vikosi SMZ wakishiriki katika hafla ya kuadhimisha Miaka 54 ya Mapinduzi Zanzibar.
BAADHI ya Wanafunzi na Vijana walioshiriki sherehe za maadhimisho ya Miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar wakishiriki katika hafla ya chakula maalum cha mchana kilichoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, katika kambi ya KVZ Mtoni Zanzibar.
WAZIRI wa Nchi na Afisi ya Rais Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Issa Haji Gavu akitowa neno la shukrani wakatika kumalizika kwa Hafla ya Chakula cha Mchana kilichoandaliwa na Rais wa Zanzinar kwa ajili yao kilichofanyika katika Kambi ya Vikosi vya KVZ Mtoni Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Viongozi wengine wa Serikali wakiitikia dua baada ya kumalizika hafla ya chakula cha mchana kilichofanyika katika Viwanja vya Kambi ya KVZ Mtoni Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakizungumza baada ya kumalizika kwa hafla ya chakula cha mchana a Vijana hao, katika viwanja vya Kambi ya KVZ Mtoni
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamen Shein, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akiwa katika picha ya pamoja na Vijana walioshiriki Sherehe za Miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika Uwanja wa Amaan 12-1-2018.


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamen Shein, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akiwa katika picha ya pamoja na Vijana walioshiriki Sherehe za Miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika Uwanja wa Amaan 12-1-2018.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na kuagana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi baada ya kumalizika hafla hiyo ya kachula maalum kilichoandaliwa kwa ajali yao katika Kambi ya KVZ Mtoni Zanzibar.








RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar baada ya kumaliza hafla ya chakula cha mchana kilichoandaliwa kwa ajili ya Vijana hao katika Viwanja vya KVZ Mtoni
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Katibu wa Halaiki Zanzibar Ali Mohammed Bakari, alipowasili katika viwanja vya Kikosi cha KVZ Mtoni kuhudhuria hafla hiyo.

VIJANA wa Bendi ya Chipukizi wakitoa burudani wakati wahafla ya chakula cha mchana kilichoandaliwa kwa ajili ya Vijana na Wanafunzi walioshiriki katika sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi Zanzibar
BAADHI ya Wanafunzi na Vijana walioshiriki sherehe za maadhimisho ya Miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar wakishiriki katika hafla ya chakula maalum cha mchana kilichoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, katika kambi ya KVZ Mtoni Zanzibar.

Picha na Ikulu
 
Support by Tone multimedia company Limited
Copyright © 2012. Zanzibar Yetu - All Rights Reserved
Designed by by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa