WAZANZIBARI WAISHIO TORONTO WAILAANI ZANZIBAR !!!
- Inayolaaniwa ni Nightclub ya Toronto yenye jina la ZANZIBAR!
- Mayor Rob Ford wa Toronto kupelekewa petition
“Wazanzibari wanaoishi katika mji wa Toronto, Canada, pamoja na vitongoji vyake, kila siku wanakasirishwa sana na kuilaani ZANZIBAR”. Hayo yalisemwa leo na Bw. Hassan Othman ambae ni Katibu wa ZACADIA. ZACADIA (Zanzibar-Canadian Diaspora Association) ni Jumuia ya Wazanzibari wanaoishi nje ya Zanzibar katika nchi ya Canada na ni chombo muhimu kinachowaunganisha Wazanzibari wote wanaoishi ughaibuni Canada.
ZANZIBAR inayolaaniwa na hawa Wazanzibari ni ya Toronto, kwani kwa Toronto neno ZANZIBAR ni jina la NIGHTCLUB moja maarufu sana kwa mambo ya ufuska, ukahaba na ngono ambayo ipo katikati ya huu mji kwenye mtaa wa Yonge (# 359) unayoigawa Toronto pande mbili - Mashariki na Magharibi. Zanzibar Nightclub inamambo machafu tele ndani yake na imekuwa ikifanya biashara hii kwa muda mrefu sana - kwa bahati mbaya tokea Zanzibar ipate Uhuru wake - 1963.
A strip club in the heart of Toronto named after the beautiful Islands of ZANZIBAR
- this deeply enrages Zanzibaris in Toronto!
- this deeply enrages Zanzibaris in Toronto!
Kusudio la Wazanzibari hawa ni kupeleka petition huko City Hall kwa Mayor wa Jiji la Toronto Bw. Rob Ford ili hii klabu ya mambo ya ufuska isipate licence chini ya jina la nchi yao tukufu na takatifu ya Zanzibar.
“Sio kama mambo haya hakuna huko kwetu Zanzibar hasa kwa siku hizi, lakini linalotusikitisha sisi ni kuwa, the only thing Torontonians know about our country (Zanzibar) is this nightclub. To them, the word ZANZIBAR is synonymous with prostitution. Kama hii klabu ingelikuwa huko Dar-Es-Salaam au Nairobi basi ingelikuwa sio kitu, kwani Zanzibar inajulikana kote huko kuwa ni nchi ya ki-Mapinduzi, lakini kwa hapa Toronto tunajulikana kama ni nchi ya upuuzi kutokana na sura mbaya hii klabu inayotupa”, alielezea Mzanzibari mmoja kwa masikitiko makubwa huku akitikisa kichwa chake.
Kutoka Zanzibarnikwetublog



0 comments:
Post a Comment