Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Ujumbne wa Kamapuni ya Kimataifa ya Miundo mbinu kutoka nchini India Hapo Ofisi ya Jimbo la Kitope Kinduni Wilaya ya Kaskazini ‘B’ Mkoa Kaskazini Unguja.
Mwenyekiti wa Kampuni ya Kimataiya ya Miundo mbinu kutoka Nchini India Balozi Vidya Bushushan Son na Ujumbe wake akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hapo Ofisi ya Jimbo la Kitope Kinduni Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Othman Kahmis Ame- Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.
Kampuni ya Kimataifa inayojishughulisha na Masuala ya Miundo Mbinu kutoka Nchini India inaendelea na utaratibu wa kuangalia Mipango yao zaidi katika kuongeza nguvu za Uwekezaji Barani Afrika.
Kauli hiyo imetolewa na Ujumbe wa Viongozi wa juu wa Kampuni hiyo ulipofanya mazungumzo na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Hapo Ofisi ya Jimbo la Kitope iliyopo Kinduni Wilaya ya Kaskazini ‘B’ Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Mwenyekiti wa Kampuni hiyo Balozi Vidya Bhushan Soni amemueleza Balozi Seif kwamba zaidi ya Dola za Kimarekani Bilioni 5.4 zimetengwa katika Bajeti ijayo kwa ajili ya kushughulikia Miradi mbali mbali Barani Afrika.
Amesema Kampuni hiyo tayari imeshawekeza kwenye miradi ya Umeme na uzalishaji wa Sukari katika Nchi za Ethiopia na Msumbiji lengo likiwa ni kusaidia msukumo wa Maendeleo barani Afrika.
“ Mtazamo wetu hivi sasa ni kuelekeza nguvu zaidi katika Mataifa ya Sudan, Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Tanzania na baadaye Kenya na Uganda”. Alisisitiza Balozi Vidya.
Balozi Vidya ameeleza kwamba Taasisi yake inaangalia utaratibu wa kuunga mkono jitihada za Mamlaka ya Maji Zanzibar { ZAWA } katika mpango wa usambazaji maji kwa Wananchi.
Hali kadhalika Balozi Vidya amemueleza Balozi Seif kwamba mkazo zaidi utawekwa katika Miradi ya Mawasiliano, Maji, Umeme pamoja na Uzalishaji wa Sukari.
Naye Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameueleza Ujumbe wa Kampuni hiyo ya Kimataifa ya Miundo Mbinu Nchini India kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imelenga katika uimarishaji wa Viwanda vidogo vidogo vya matunda.
Balozi Seif amesema Zanzibar imebarikiwa kuwa na Matunda mengi lakini kinachokosekana ni ukosefu wa Utaalamu pamoja na Viwanda katika usindikizaji wa mazao hayo.
0 comments:
Post a Comment