Home » » Maziko Ya Aliyekuwa Mwanasheria Wa Kwanza Zanzibar

Maziko Ya Aliyekuwa Mwanasheria Wa Kwanza Zanzibar


 Mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzbar marehemu Abeid Aman Karume Mama Fatma Karume alie kushoto akiwa pamoja na Bi Yvon Mke wa aliekuwa Jaji Mkuu wa Mwanzo wa Zanzibar Marehemu Wolfgang Dourado katika kanisa la Minara miwili Shangani mjini Zanzibar katika ibada maalum ya kuuwaga mwili wa Marehem Dourado.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi akiwa pamoja na Viongozi mbalimbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuuwaga mwili wa Marehemu Wolfgang Dourado aliekuwa Jaji Mkuu wa Mwanzo wa Zanzibar katika kanisa la Minara miwili Shangani mjini Zanzibar.

 Balozi Ali Karume akimfariji Mjane wa aliekuwa Jaji Mkuu wa Mwanzo wa Zanzibar Wolfgang Dourado Bi Yvon Dourado katika kanisa la Minara miwili Shangani mjini Zanzibar.

 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi akichota Mchanga kwa ajili ya kwenda kutia katika kaburi la aliekuwa Jaji Mkuu wa Mwanzo wa Zanzibar Wolfgang Dourado aliezikwa huko kwerekwe katika Makaburi ya Wakristo.

 Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohd Shein akienda kutia mchanga katika Kaburi la aliekuwa Jaji Mkuu wa Mwanzo wa Zanzibar Wolfgang Dourado aliezikwa huko kwerekwe katika Makaburi ya Wakristo
 -Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohd Shein akiweka Shada la Mauwa katika Kaburi la aliekuwa Jaji Mkuu wa Mwanzo wa Zanzibar Wolfgang Dourado aliezikwa huko kwerekwe katika Makaburi ya Wakristo.
 -Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohd Shein akimpa Mkono wa pole Bi Yvon Dourado Mjane wa aliekuwa Jaji Mkuu wa Mwanzo wa Zanzibar Marehemu Wolfgang Dourado aliezikwa huko kwerekwe katika Makaburi ya Wakristo

PICHA ZOTE NA YUSSUF SIMAI MAELEZO ZANZIBAR.20/03/2012.

0 comments:

Post a Comment

 
Support by Blogs za Mikoa Tanzania
Copyright © 2012. Zanzibar Yetu - All Rights Reserved
Designed by by Blogs za Miikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa