Home » » GRAND MALT MDHAMINI MKUU LIGI KUU YA ZANZIBAR

GRAND MALT MDHAMINI MKUU LIGI KUU YA ZANZIBAR

Waziri wa Habari,Utamaduni,Utalii na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,Mh Ally Mbarouk (kulia) akipena mkono na Mkurugenzi wa Masoko wa TBL,Kushilla Thomas wakati wakibadilisha mikataba ya udhamini wa ligi kuu ya soka ya Zanzibar (ikiliwa ni mkataba wa miaka mitatu) kupitia kinywaji cha Grand Malt wakati wa hafla fupi iliyofanyika leo kisiwani Zanzibar.Katikati ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Mh. Abdallah Hassan Jihad.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Utalii na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,Mh. Ally Mbarouk (wa tatu kushoto) akikadhi Mkataba huo kwa Kaimu Rais wa ZFA,Ally Mohamed (wa pili kulia) ukiwa ni mkataba wa miaka mitatu ya udhamini kutoka kwa TBL kupitia Kinywaji chake cha Grand Malt wakati wa hafla fupi iliyofanyika leo kisiwani Zanzibar.Wengine pichani toka kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko wa TBL,Kushilla Thomas,Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Mh. Abdallah Hassan Jihad na kulia ni Meneja wa Kinywaji cha Grand Malt,Consolata Adam.

Kinywaji maarufu cha Grand Malt leo kimethibitisha rasmi kudhamini ligi kuu ya soka visiwani Zanzibar kwa msimu utakaonza mwezi Agosti mwaka 2012.

Akizungumza katika makabidhiano ya mkataba wa udhamini huo yaliyofanyika katika hoteli ya Bwawani, Zanzibar; Meneja wa kinywaji cha Grand Malt Bi Consolata Adam alisema; Grand Malt ni kinywaji kisicho na kilevi, ambacho kimetokea kupendwa sana na watumiaji kote Tanzania Bara na hapa Zanzibar. 

Leo tunayo furaha kubwa sana kutangaza kuwa kinywaji hiki mkipendacho cha Grand Malt kimekubali kwa heshima na taadhima kuchukua jukumu la kuendeleza soka la Zanzibar kwa kudhamini Ligi kuu ijulikanayo kama “Zanzibar Premier League”. 

Kwetu sisi, hii ni mojawapo ya njia tutakazozitumia kurejesha fadhila zetu kwa wazanzibari kwani mmekipokea kinywaji hiki na kinaendelea kukua kwa kasi, nasi hatuna budi kusema Ahsanteni sana kupitia ushirikiano huu tunaouanza katika kuhakikisha tunaendeleza soka la Zanzibar kupitia udhamini huu.

Akielezea udhamini huo, meneja masoko wa Grand Malt Bw. Fimbo Butallah alisema; Tumesaini mkataba wa miaka mitatu kuidhamini ligi kuu ya Zanzibar kupitia kinywaji cha Grand Malt. Mkataba huu unaanza mwaka huu 2012 kwa msimu wa ligi utakaoanza mwezi Agosti hadi mwaka 2014. 

Kwa mwaka huu wa kwanza Grand Malt itatoa shilingi 140,000,000/- ambapo fedha hizi zitatumika kwa mahitaji mbali mbali ya ligi kama vile mahitaji ya Timu shiriki kwa usafiri, chakula na malazi, vifaa vya michezo na zawadi kwa washindi. 

Kufuatia udhamini huu ambao ni zaidi ya asilimia 70 ya mahitaji ya kuendesha ligi, sasa Grand Malt inawaasa wadau wote wa soka hapa Zanzibar kushirikiana kwa pamoja ili tuhakikishe kuwa tunaleta mabadiliko makubwa katika tasnia hii.

Nae Makamu wa Raisi wa Chama cha Mpira Zanzibar (ZFA); Bw. Ally Mohamed alisema; Tukio hili la leo ni matunda ya mchakato mzima ulioongozwa na Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo ya Zanzibar na uongozi wa Chama cha mpira Zanzibar (ZFA). 

Ambao walitoa fursa hii kwa Grand Malt, kuweza kudhamini ligi yetu ya Zanzibar. Fursa hii inatokana na ukweli kwamba hawa wenzetu wana uzoefu mkubwa katika kuendeleza soka na michezo mbalimbali. Kwa Udhamini huu Grand Malt sasa inapewa heshima ya kubeba jina la ligi hii na hivyo itajulikana kama “Grand Malt Premier League”.

Tuna imani kubwa kuwa ushirikiano huu tunaouanza sasa na Grand Malt utaleta ufanisi mkubwa katika ligi yetu. Kwa niaba ya ZFA tunaahidi kuzingatia masharti na matakwa ya mkataba, na kutoa ushirikiano thabiti katika kuendeleza michezo hapa Zanzibar. 

Pia tunatoa fursa kwa wadau wengine kujitokeza ili wachukue nafasi ya wadhamini wenza ili kuongeza nguvu zaidi katika hiki tulichopata toka Grand Malt.

0 comments:

Post a Comment

 
Support by Blogs za Mikoa Tanzania
Copyright © 2012. Zanzibar Yetu - All Rights Reserved
Designed by by Blogs za Miikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa