Home » » PICHA ZA MATUKIO YA KUWASILI, KUAGWA MWILI WA MAREHEMU PAMOJA NA MAZISHI BRIGEDIA GENERALI ADAM MWAKANJUKI ZANZIBAR

PICHA ZA MATUKIO YA KUWASILI, KUAGWA MWILI WA MAREHEMU PAMOJA NA MAZISHI BRIGEDIA GENERALI ADAM MWAKANJUKI ZANZIBAR


Wanajeshi wa JWTZ  wakiwa wamebeba mwili wa Marehemu Brigedia Jenerali Adam Mwakanjuki mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Abeid Karume Zanzibar kutokea Dar es Salaam kwa ajili ya mazishi.
 Wanafamilia wa Marehemu Brigedia Jenerali  Adam Mwakanjuki wakiwa na huzuni baada ya kuwasili kwa mwili wa marehemu huyo huko katika Uwanja wa Ndege wa Abeid Karume Zanzibar.
 Wanafamilia wa Marehemu Brigedia Jenerali  Adam Mwakanjuki wakiwa na huzuni baada ya kuwasili kwa mwili wa marehemu huyo huko katika Uwanja wa Ndege wa Abeid Karume Zanzibar.
Mke wa marehemu Brigedia Jenerali Mwakanjuki Ikupa Abel Mwasongwe akiwa pamoja na Familia yake huko katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la zamani ambako mwili huo unapoagwa.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohammed Shein akisaini kitabu cha maombolezo huko katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la zamani ambako mwili huo ulipoagwa.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd akisaini kitabu cha maombolezo cha Marehemu Brigedia Jenerali Mwakanjuki huko katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la zamani ambako mwili huo ulipoagwa.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Pandu Ameir Kificho akisaini kitabu cha maombolezo huko katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la zamani ambako mwili huo ulipoagwa.
Rais Mstaafu wa Zanzibar Aman Abeid Karume akisaini kitabu cha maombolezo cha Marehemu Brigedia Jenerali Mwakanjuki huko katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la zamani ambako mwili huo ulipoagwa.

Mke wa Rais Mstaafu wa Zanzibar Shadya Karume akisaini kitabu cha maombolezo cha Marehemu Brigedia Jenerali Mwakanjuki huko katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi wa zamani Kikwajuni ambako mwili huo ulipoagwa.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohammed Shein akiuaga mwili wa Marehemu Brigedia Jenerali Adam Mwakanjuki katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la zamani Kikwajuni.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd akiuaga mwili wa Marehemu Brigedia Jenerali Adam Mwakanjuki katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la zamani Kikwajuni.
Rais Mstaafu wa Zanzibar Aman Abeid Karume na Mke wake Shadya wakiuaga mwili wa Marehemu Brigedia Jenerali Mwakanjuki huko katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la zamani ambako mwili huo ulipoagwa.(PICHA ZOTE NA Yussuf Simai-Maelezo Zanzibar 22-04-2012).

 Wanajeshi wa JWTZ wakiliweka jeneza katika kaburi kwa ajili ya Mazishi yaMarehemu Brigedia Jenerali Mstaafu Adam Mwakanjuki huko katika Makaburi ya Mwanakwerekwe Mjini Zanzibar.


 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohd Shein akitia mchanga katika Kaburi la Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu Adam Mwakanjuki huko katika Makaburi ya Mwanakwerekwe Mjini Zanzibar.


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Mohd Gharib Bilali akitia mchanga katika Kaburi la Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu Adam Mwakanjuki huko katika Makaburi ya Mwanakwerekwe Mjini Zanzibar.


 -Rais Mstaafu wa Zanzibar Dk Aman Abeid Karume akitia mchanga katika Kaburi la Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu Adam Mwakanjuki huko katika Makaburi ya Mwanakwerekwe Mjini Zanzibar.

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohammed Shein akiweka shada la Maua katika Kaburini baada ya maziko huko katika Makaburi ya Mwanakwerekwe Mjini Zanzibar.
-

 PICHA ZOTE NA YUSSUF SIMAI MAELEZO ZANZIBAR.

0 comments:

Post a Comment

 
Support by Blogs za Mikoa Tanzania
Copyright © 2012. Zanzibar Yetu - All Rights Reserved
Designed by by Blogs za Miikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa