Home » » JESHI LA POLISI ZANZIBAR LASITISHA MHADHARA WA UAMSHO

JESHI LA POLISI ZANZIBAR LASITISHA MHADHARA WA UAMSHO



Na Mwandishi wa Jeshi la Polisi Zanzibar
JESHI la Polisi Zanzibar limepiga marufuku maandamano na mihadhara ya aina yoyote visiwani hapa hadi hapo itakapotangazwa tena.
Taarifa
ya Afisa Habari Mkuu wa Jeshi la Polisi Zanzibar Inspekta Mohammed
Mhina, imesema kuwa hatua hiyo inatokana na agizo la Serikali la
kusitisha shughuli zote za mikusanyiko ya vikundi vya kidini vikiwemo
vile vyenye usajili na ambavyo havina ili kuepusha uvunjifu wa amani.
Akisisitiza
msimamo huo wa Jeshi la Polisi, Kamishna wa Polisi Zanzibar CP Mussa
Ali Mussa, amesema Jeshi la Polisi litachukua hatua kali kwa mtu ama
kikundi chochote kitakachokaidi agizo hilo kwa lengo la kudumisha amani
na usalamawa viisiwa hivyo.
Kamishna
Mussa amesema Jeshi la Polisi limelazimika kutoa msisitizo huo kufuatia
taarifa za viongozi wa kikundi cha Uamsho kuwatangazia wananchi kuwa
kesho wangefanya mhadhara kwenye viwanja vya Lumumba kinyume na maagizo
ya Serikali.
Amewataka
Wananchi wakiwemo waumini wa dini zote kutojitokeza kushiriki mhadhara
huo na mihadhara mingine itakayotangazwa katika kipindi hiki cha
marufuku ya mikusanyiko ya aina hiyo.
Jana
akizungumza na Waandishi wa Habari mjini Zanzibar, Kiongozi wa Kikundi
cha Uamsho Sheikhe Farid Hadi, alisema wangefanya mhadhara mkubwa hiyo
kesho jioni na kufanya maandamano Jumanne ya Juni 26, mwaka huu.

0 comments:

Post a Comment

 
Support by Blogs za Mikoa Tanzania
Copyright © 2012. Zanzibar Yetu - All Rights Reserved
Designed by by Blogs za Miikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa