MOHAMED ABOUD MOHAMED [MBM] WAZIRI WA NCHI OFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR
Mheshimiwa Spika;
Kwa
heshima naomba kuchukua nafasi hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa
kutujaalia kukutana hapa leo tukiwa wazima na wenye afya njema. Pili,
naomba nichukue nafasi hii adhimu kukushukuru wewe Mheshimiwa Spika
kutupatia fursa hii adhimu ili kuwasilisha mbele ya Baraza lako Tukufu
taarifa ya maafa ya kuzama kwa meli ya MV. Skagit iliyotokea katika
bahari ya Chumbe tarehe 18.07.2012.
1.0 Utangulizi
Mheshimiwa Spika,
Meli
ya MV. Skagit ilitengenezwa nchini Marekani mwaka 1989 na imesajiliwa
Zanzibar tarehe 25/10/2011, na kupewa nambari ya usajili 100144. Meli
hiyo ina uzito wa GRT96 ambayo inamilikiwa na kampuni ya Seagull Sea
Transport Limited ya Zanzibar.
Mheshimiwa Spika,
Mnamo
tarehe 18.07.2012 majira ya saa saba na nusu za mchana ilipatikana
taarifa ya ajali ya kuzama kwa meli ya MV. Skagit katika bahari ya
chumbe nje kidogo ya mji wa Zanzibar. Meli hiyo ilikuwa katika safari
zake za kawaida ya kutoka Dar-es-Salaam kuja Zanzibar.
Kwa mujibu
wa manifest ya abiria iliyowasilishwa na wamiliki wa meli kwa Mamlaka
ya Bandari Tanzania (Tanzania Ports Authority-TPA) na Mamlaka ya Usafiri
wa Baharini na Nchi Kavu Tanzania (Surface and Marine Transport
Authority-SUMATRA), meli hiyo ilikuwa imechukua jumla ya watu 290
wakiwemo abiria watu wazima 250, watoto 31 na mabaharia 9.
Mheshimiwa Spika,
Taarifa
hii inaelezea kwa kina juu ya hali halisi ya tukio pamoja na hatua zote
zilizochukuliwa kuanzia tarehe 18/07/2012 hadi hivi sasa.

Mara baada ya
tukio hili, Kamati ya Kukabiliana na Maafa ya Taifa ilikutana kwa ajili
ya kuweka mikakati ya hatua za kuchukua pamoja na kuandaa taarifa rasmi
ya Serikali kwa wananchi kupitia vyombo vya habari. Aidha, Baraza la
Mapinduzi lilikaa usiku wa tarehe 18.07.2012, na kutoa maagizo juu ya
hatua za kuchukua ikiwemo kuwepo kwa matayarisho katika hospitali ya
mnazi Mmoja ya kupokea majeruhi, kutayarisha eneo la Maisara kwa ajili
ya mapokezi na utambuzi wa maiti; kutayarisha eneo la kuzika miili ya
marehemu huko Kama; kuweka takwimu sahihi za majeruhi na waliofariki
katika ajali hiyo; pamoja na kutolewa kwa taarifa rasmi ya hali ya
uokozi iliyokuwa inaendelea.Kusoma Kauli nzima Bofya na Endelea........>>>>

0 comments:
Post a Comment