Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiendelea
kukemea uvuvi haramu nchini alipokuwa akizungumza na wananchi wa Kijiji
cha Marumbi.
Kulia ni Mwkilishi wa Jimbo la Chwaka Mh. Issa Haji Ussi na Kushoto ya
Balozi ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mh. Abdulla Mwinyi.
kukemea uvuvi haramu nchini alipokuwa akizungumza na wananchi wa Kijiji
cha Marumbi.
Kulia ni Mwkilishi wa Jimbo la Chwaka Mh. Issa Haji Ussi na Kushoto ya
Balozi ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mh. Abdulla Mwinyi.
Mvuvi Bwana Ali Bakari Othman wa Kijiji cha Mrumbi akipokea msaada wa
shilingi 6,000,000/- kutoka kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Balozi Seif Ali Iddi kwa ajili ya ununuzi wa nyavu za Wavuvi wa kijiji
hicho zilizoharibiwa tarehe 28 Febuari mwaka 2012.
Bwana Ufuso Haji haji akiwakilisha mawazo ya Wananchi wa Marumbi katika
kuelezea kadhia zinazowakabili katika suala zima la uvuvi haramu ndani
ya ghuba ya Chwaka.
kuelezea kadhia zinazowakabili katika suala zima la uvuvi haramu ndani
ya ghuba ya Chwaka.
Baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Marumbi wakimsikiliza Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hayupo pichani alipokuwa
akizungumza nao kufuatia kadhia iliyowapata wavuvi wa Kijiji hicho kwa
kuchomewa mashua zao mbili za Uvuvi tarehe 28/2/201
Mkurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania BOT Tawi la Zanzibar Bwana Joseph
Mhando akiwasilisha mchango wa Shilingi 10,000,000/- kwa Makamu wa Pili
wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwa ajili ya mfuko wa Maafa
hapo Baraza la Wawakilishi Mbweni Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
2.Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana
na Uongozi wa Benki Kuu ya Tanzania BOT uliofika ofisini kwake Baraza la
Wawakilishi Mbweni kutoa mkono wa pole kufuatia ajali ya meli ya M.V.
Skagiti hivi karibuni.
--
Usimamizi mbovu unaoendelea kufanywa
na Baadhi ya Viongozi wa Serikali ikiwemo uzuiwaji wa vikosi vya doria
kufanya doria umepelekea kuongezeka kwa uvuvi haramu katika ghuba ya
Chwaka.
na Baadhi ya Viongozi wa Serikali ikiwemo uzuiwaji wa vikosi vya doria
kufanya doria umepelekea kuongezeka kwa uvuvi haramu katika ghuba ya
Chwaka.
Kauli hiyo imetolewa na Wananchi wa Kijiji cha Marumbi walipokuwa
wakielezea matatizo wanayopambana nayo mbele ya Makamu wa Pili wa Rais
wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipokutana nao kujua tatizo la kiini
cha mgogoro usiopunguwa miaka 31 sasa ndani ya ghuba hiyo.
Bwana Ufuso Haji Haji akiwakilisha Wananchi hao katika mazungumzo hayo
alisema sheria za uvuvi zipo lakini kinachosikitisha ni kuona baadhi ya
Viongozi wa Serikali kuzifumbia macho na hatimae kuwaachia baadhi ya
wavuvi kuendeleza uvuvi haramu.
Alisema wakati wanakijiji wanapigania kudhibiti uvuvi haramu wapo
Viongozi wa Serikali wanaotumia nyadhifa na vyombo vyao vya uvuvi kuwapa
wavuvi wengine wasiojali udhibiti wa hali hiyo.
“ Huu ni wakati mgumu sasa kwa vile tumefikia wakati tukiamini kwamba
Serikali inajaribu kutuchezea wanakijiji wa marumbi na ndio maana
tumefikia hatua ya kutokubaliana na lolote. Vyenginevyo labda aje Rais
wa Nchi hapa”. Alisisitiza Bwana Ufuso.
Alisisitiza kwamba Wananchi wa Marumbi hawatakuwa tayari kwa lolote hadi
tatizo lao la kuharibiwa Mashua zao zilizochomwa moto Tarehe 28/2/2012
litakapotatuliwa.
Akitoa nasaha zake kwa Wananchi hao wa Marumbi Makamu wa Pili wa Rais
wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amekiagiza Kikosi cha Kuzuia Magendo
KMKM kuanzia sasa kufanya kazi zake za doria kwa mujibu wa taratibu
zilizowekwa.
Balozi Seif amewaahidi Wananchi hao kwamba akiwa mtendaji Mkuu wa
Serikali atahakikisha anasimamia kwa nguvu zote kukabiliana na tatizo la
uvuvi haramu hapa Nchini.
“ Kuanzia sasa tutakwenda kutoa amri kwa KMKM ifanye wajibu wake wa
kulinda uvuvi haramu unaofanywa na wavuvi wakorofi”. Alisisitiza Balozi
Seif .
Alisema kama wapo Viongozi wanaoruhusu uvuvi haramu wajue kwamba
wanafanya makosa makubwa .
Balozi Seif katika Mkutano huo amekabidhi jumla ya Shilingi 6,000,000/-
kwa ajili ya kusaidia wavuvi walioharibiwa nyavu zao na kuahidi
atazungumza na Viongozi wenzake ili kulipatia ufumbuzi tatizo la mashua
zao mbili zilizo haribiwa mapema mwaka huu.
Mapema asubuhi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
alipokea mchango wa maafa wa shilingi milioni kumi {10,000,000/- }
kutoka kwa Uongozi wa Benki Kuu ya Tanzania { BOT }.
Mchango huo umewasilishwa na Mkurugenzi wa BOT Tawi la Zanzibar Nd.
Joseph Mhando kwa niaba ya Gavana na Uongozi mzima wa Makao Makuu ya
Benki hiyo yaliyopo Mjini Dar es salaam.
Akiwasilisha mchango huo Nd. Mhando alisema uongozi wa Benki hiyo
umefarajika na hatua zilizochukuliwa na Serikali pamoja na Vikosi vya
Ulinzi kwa usimamizi mzuri uliofanikisha zoezi zima la uokozi wa Watu
waliokuwemo kwenye Meli iliyozama ya M.V. Skagit hivi karibuni.
“ Tunastahiki kuipongeza Serikali kupitia washirika wake hasa Vikosi
vya Ulinzi na Uokozi kwa kuendesha zoezi zima la uokozi katika
mazingira magumu kabisa”. Alisisitiza Ndugu Joseph.
Mkurugenzi huyo wa Benki Kuu ya Tanzania Tawi la Zanzibar amewaombea
malazi mema wale waliotangulia mbele ya haki na kuwatakia maisha ya
furaha wale waliookoka kwenya ajali hiyo mbaya.
Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali
Iddi alisema Serikali imesikitishwa na ajali hiyo kwa vile imezigusa
familia za pande zote za Muungano.
“ Janga hili liliikumba Tanzania yote kwa sababu waliosafiri na chombo
hicho walikuwa na asili ya pande zote za Tanzania”. Alifafanua Balozi
Seif Ali Iddi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif aliuelezea ujumbe wa
Uongozi wa Benki hiyo ya Tanzania kwamba Baraza la Usalama la Taifa
limeshaamua na kuagiza Meli zote zinazoagizwa au kununuliwa ni lazima
zipate ridhaa ya kukubalika Kitaalamu kutoka kwa Mamlaka zinazosimamia
usafiri wa Baharini.
Alisema hadi sasa maiti zilizopatikana kutokana na ajali hiyo ya Meli
zimefikia watu 136, waliookolewa hai ni Watu 146, watu wanane bado
hawajapatikana kwa mujibu wa idadi ya abiriwa 290 waliokuwa
wameandikishwa kusafiri na Meli hiyo ya M.V.Skagit kutoka Bandari ya Dar
es salaam kuelekea Zanzibar.
Na
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais
wa Zanzibar
wa Zanzibar
0 comments:
Post a Comment