Home » » Rais wa Zanzibar Dk Ali Shein Afuturisha Mkoa wa Mjini Magharibi

Rais wa Zanzibar Dk Ali Shein Afuturisha Mkoa wa Mjini Magharibi

 Baadhi
ya Wananchi na Waumini wa Dini ya Kiislamu wa Mkoa wa Mjini Magharibi
wakianza kufutari kwa kunywa madafu kabla ya kula futari jana
walipoalikwa katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanibar na Rais wa Zanzibar
na Mwenyekiti wa Baraza La Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,ikiwa ni
kawaida yake kuwaalika Wananchi wa Mkoa huo kila ifikapo mwezi kama huu
kwa futari maalum.
  Baadhi
ya Viongozi na Wananchi Waumini wa Dini ya Kiislamu wa Mkoa wa Mjini Magharibi,wakiwa katika chakula cha Futari katika Mwezi mtukufu wa Ramadhan,iliyoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,katika viwanja vya Ikulu Mjini
Zanzibar
  Baadhi
ya Wananchi na Waumini wa Dini ya Kiislamu wa Mkoa wa Mjini Magharibi
wakiwa katika futari iliyoandaliwa jana ,katika viwanja vya Ikulu Mjini
Zanibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza La Mapinduzi Alhaj
Dk.Ali Mohamed Shein,ikiwa ni kawaida yake kuwaalika Wananchi wa Mkoa
huo kila ifikapo mwezi kama huu kwa futari maalum.
Baadhi ya Akina mama wa Mkoa wa Mjini Magharibi wakiwa katika chakula cha Futari,iliyoandaliwa na Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,katika
viwanja vya Ikulu ya Zanzibar.
  Baadhi ya Akina mama wa Mkoa wa Mjini Magharibi wakiwa katika chakula cha Futari,iliyoandaliwa na Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,katika
viwanja vya Ikulu ya Zanzibar.
 Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, (wa pili kushoto) akijumuika na
akinamamawa wa Mkoa wa Mjini Magharibi katika Chakula cha Futari
iliyoandaliwa kwa wananchi hao na Rais wa Zanzibar Alhaj Dk.Ali Mohamed
Shein, katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar, (wengine kulia) Mama
Shadiya Karume, Mama Pili Balozi Seif na Waziri wa Muungano Samia Suluhu
Hassan, (kushoto).
 Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed
Shein,(wa pili kulia) akijumuika na wananchi pamoja na Viongozi wa Mkoa
wa Mjini Magharibi katika Futari, aliyowaandalia wananchi hao katika
viwanja vya IKulu ya Mjini Zanzibar jana, (kulia) Mkuu wa Mkoa wa Mjini
Magharibi Abdalla Mwinyi Khamis,Rais Mstaafu wa Zanzibar Dk.Amaan Abeid
Karume,(kushoto) na Mufti wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi.
 Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed
Shein, akisalimiana na Viongozi na wananchi wa Mkoa wa Mjini Magharibi
baada ya kufutari nao pamoja jana katika futari aliyowaandalia katika
viwanja vya IKulu ya Mjini Zanzibar.
 Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed
Shein, na Mkewe Mama Mwanamwema Shein, wakisalimiana na Viongozi na
Wananchi wa Mkoa wa Mjini Magharibi baada ya kumalizika Futari
waliyowaandalia katika Viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar.
 Mke
wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama
Mwanamwema Shein, (kulia) akisalimiana na mke wa Rais mstaafu wa
Zanzibar Mama Shadya Karume, baada ya Futari iliyoandaliwa kwa wananchi
wa Mkoa wa Mjini Magharibi na Rais wa Zanzibar Alhaj Dk.Ali Mohamed
Shein, katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar.
Picha na Ramadhan Othman, Ikulu-Zanzibar



0 comments:

Post a Comment

 
Support by Blogs za Mikoa Tanzania
Copyright © 2012. Zanzibar Yetu - All Rights Reserved
Designed by by Blogs za Miikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa