Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DKT Ali Mohamed Shein amemteuwa Abdulsalam Issa Khatibu kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo cha Kilimo, Kizimubani.
Kwa mujibu wa Taarifa kutoka kwa Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano Ikulu Hassan Khatib imeeleza kuwa Abdulsalam anachukuwa nafasi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza hilo Makame Salum ambaye muda wake wa Kikazi ulimalizika.
Abdulsalam Issa aliwahi kuwa Mbunge wa CCM wa Jimbo la Makunduchi na ni Mtaalamu wa mambo ya Kilimo ambaye alifanyakazi ndani na nje ya nchi katika Mashirika yakimataifa.
Aidha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DKT Ali Mohamed Shein amemteuwa Mayasa Salim Ali kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Tiba Asili na Mbadala Zanzibar.
Uteuzi huo umeanza tarehe 27Septemba 2012.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR
29/9/2012

0 comments:
Post a Comment