Home » » MAJENGO ZANZIBAR KUWA RAFIKI KWA WALEMAVU

MAJENGO ZANZIBAR KUWA RAFIKI KWA WALEMAVU

na Mauwa Mohammed, Zanzibar
SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar inakusudia kuanzisha sheria itakayozingatia ubora wa majengo ambayo yatakuwa rafiki kwa watu wenye ulemavu nchini.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Mwenyekiti wa Kamati wa Mfuko wa Watu wenye ulemavu, Nassor Ahmed Mazrui, alipozungumza na waandishi wa habari mjini hapa.
Alisema kamati na baraza la watu wenye ulemavu litaandaa sheria ndogondogo, ili majengo yote yatakayojengwa na serikali na watu binafsi yazingatie mahitaji ya watu wenye ulemavu.
Mbali na hilo, alisema kamati hiyo itaandaa harambe ya kuchangia mfuko wa watu wenye ulemavu Septemba 28 mwaka huu, ili kuondoa changamoto zinazowakabili watu hao.
Alisema mfuko huo utawasaidia watu weye ulemavu kupata ruzuku kwa wale wasioweza kufanya kazi na kuwapatia mitaji kwa wale watakaokuwa na miradi mbali ya kuwapatia kipato.
Chanzo: Tanzania Daima

0 comments:

Post a Comment

 
Support by Blogs za Mikoa Tanzania
Copyright © 2012. Zanzibar Yetu - All Rights Reserved
Designed by by Blogs za Miikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa