Home » » NGWASUMA KUKAMUA ZANZIBAR IJUMAA

NGWASUMA KUKAMUA ZANZIBAR IJUMAA

na Mwandishi wetu
BENDI ya muziki wa dansi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’, inatarajiwa kufanya shoo ya nguvu kwenye Bwalo la Maofisa wa Polisi mjini Zanzibar, keshokutwa.
Katika shoo hiyo, bendi hiyo itatambulisha nyimbo na mitindo mipya katika mji huo ulioadimika burudani za muziki wa dansi kwa muda mrefu, hivyo kuwa sehemu ya kuonyesha makali yao.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa bendi hiyo, Kelvin Mkinga, alisema kwamba vijana wake wakiongozwa na Rais wa Vijana, Nyosh el Sadaat, watafanya mambo makubwa kwa ajili ya kuwapa burudani kali wapenzi wa visiwani humo.
Alisema anaamini kuwa burudani hizo zitafurahisha watu wengi katika tasnia ya muziki wa dansi, ukizingatia wao ndio vinara na wanaotingisha katika jukwaa la dansi, licha ya kuwa na ushindani wa aina yake.
“Huu ni wakati wa kuonyesha kuwa sisi ni bendi imara na yenye mipango imara, hivyo wapenzi wetu na wadau wote visiwani humo ni wakati wao wa kuburudika Ijumaa, huku wakipata vibao vipya na vya zamani.
“Tunakwenda visiwani Zanzibar baada ya kukosekana huko kwa muda mrefu, nadhani wadau wataitumia nafasi hiyo kuingia kwa wingi na kujipatia burudani za Ngwasuma zinazoongozwa na Nyoshi,” alisema Mkinga.
Baadhi ya nyimbo zinazopendwa na wengi katika bendi hiyo ni pamoja na ‘Otilia’, ‘Heshima kwa Wanawake’, ‘Anna’, ‘Dunia Kigeugeu’ na nyinginezo.
Chanzo: Tanzania Daima

0 comments:

Post a Comment

 
Support by Blogs za Mikoa Tanzania
Copyright © 2012. Zanzibar Yetu - All Rights Reserved
Designed by by Blogs za Miikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa