Home » » MAADHIMISHO YA SIKU YA WAZEE DUNIANI (ZNZ)

MAADHIMISHO YA SIKU YA WAZEE DUNIANI (ZNZ)


 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenekiti wa Baraza la Mapinduzi Mwinyihaji Makame Mwadini akisalimiana na mmoja ya Wazee bi Raya Abdallah Masaku baada ya kuangalia vitu ambavyo wazee hao wa Sebleni wanavitengeneza katika maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani


 Baadhi ya wazee ambao wanatunzwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika nyumba za Sebleni Amani mjini Zanzibar wakiwa wanasikiliza hotuba ya mgeni rasmi (hayupo pichani)katika maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo octoba 1.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

========  ========  ======  ======
Na Khadija Khamis –Maelezo     Zanzibar    01/10/2012.

Serikali ya Mapinduzi Zanzíbar imesema kuwa imepanga sera na mikakati  ya kuwaenzi na kuwathamini wazee wote pamoja na kuwawekea jitihada za kuhakikisha wanapata mustakbali mwema wa maisha yao .

Hayo yameelezwa leo huko Nyumba za Wazee Sebleni wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Mwinyihaji Makame kwa niaba ya Rais wa Zanzíbar na Mwenykiti wa Baraza la Mapinduzi .

Alisema kuwa serikali ipo katika mchakato wa kuandaa sera ya hifadhi ya jamii ambayo itazungumzia maslahi ya makundi yote katika jamii ikiwa  ni pamoja na wazee .Aidha alisema kuwa wazee wanahitaji kuenziwa na kudhaminiwa kutokana na kuishiwa   nguvu za mwili na kukosa uwezo wa kufanya kazi.

Aidha akifahamisha kuwa jitihada za Serikali zinatarajia kufikia hatua nzuri za kuweza kuwapunguzia umaskini kwa kuwawezesha wazee wote waliyofanya kazi katika serikali na wale ambao walifanyakazi zao binafsi kuweza kuwakomboa na umasikini uliokithiri na  kufikia lengo kuu la millenium.

Dk Mwinyihaji alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzíbar imeeandaa mambo maalum kwa ajili ya wazeee ikiwemo pencheni nzuri kuimarishiwa huduma za afya ndani ya makaazi yao kwa wale wazee wanaishi makaoni  na kuweza kuimarisha ustawi wa wazee kwa  kuwawezesha kuwapa mafunzo mbali mbali ili kuwajengea uwezo wazee hao.

Nae Waziri wa Ustawi wa Jamii Maendeleo ya Vijana na Watoto Zainab Mohammed alisema kuwa anaipongeza serikali kwa kuweza kuitambua siku hii athimu ya wazee ya kuweza kuwawekea wazee misingi imara ya kuwatunza kuwaenzi na  kuwathamini . Aidha  alisema kuwa leo ni siku ya faraja Kubwa kwa kupata fursa ya kusherehekea siku hii adhimu ya wazee duniani .

“Kwani mzee ameitwa mzee kwa kuishiwa na nguvu za kujihudumia kwa kiasi kikubwa amesema’’ Waziri  Zainaab . Nae muakilishi wa shirika la Help Age Internationl Flavian Bifandimu alisema kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kufanya mabadiliko ili kusaidia majukumu kwa wazee. Pia alisema kuwa kutatua matatizo ya wazee kutasaidia kuwawekea mustakbali mzuri ili kuepukana na umaskini na omba omba wa mitaani .

Nao wazee hao waliomba serikali iwape  muakilishi wa wastaafu katika baraza la wawakilishi na bunge ili waweze kusemewa matatizo yao na wazee wanataka kushirikishwa katika vikao vya maamuzi  huduma ya afya iwe bure na wazee wanataka wasaminiwe na watambuliwe hasa na huduma ya pencheni pia iangaliwe kutokana na wakati uliopo hivi sasa .

Ujumbe wa mwaka huu wa siku ya wazee duniani ni MAISHA BORA NA HAKI KWA WAZEE WOTE  .Katika sherehe hizo wazee mbali mbali walichunguzwa afya zao na jumla ya wazee  773 waangaliwa afya zao na 321 waliweza kupatiwa miwani .
 IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR


0 comments:

Post a Comment

 
Support by Blogs za Mikoa Tanzania
Copyright © 2012. Zanzibar Yetu - All Rights Reserved
Designed by by Blogs za Miikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa