Malkia
wa Filamu ya Espinho da Rosa (the Thorn of the rose) ya Filipe
Henriques kutoka Guinea Bissau ADY de Batista akiwasili huku
akiongozana na Meneja wake Sholey Maqueta kwenye usiku maalum wa tuzo
wakati wa tamasha la 17 la ZIFF 2014 lililomalizika mwishoni mwa juma
visiwani Zanzibar kwenye viunga vya Ngome Kongwe.
Na Mwandishi wetu, Zanzibar
FILAMU
ya Espinho da Rosa (the Thorn of the rose) ya Filipe Henriques kutoka
Guinea Bissau imeondoka na tuzo tatu katika tamasha la 17 la filamu la
kimataifa la Zanzibar (ZIFF).
Tuzo hizo ni pamoja na ya Signis , tuzo ya majaji na tuzo ya fedha ya ZIFF.
Katika
tamasha hilo filamu iliyotwaa tuzo ya dhahabu ni ile ambayo ilikataliwa
kuoneshwa nchini Nigeria ilikotengenezwa ya Half of a Yellow Sun
iliyoongozwa na Biyi Bandele.
Shughuli
za utoaji tuzo ambazo zilitanguliwa na hotuba ya makamu mwenyekiti wa
kampuni ya wananchi Group ambayo brand yake ya zuku ndio inafadhili
ZIFF pamoja na tuzo zake za Swahili, zilinogezshwa na vikundi
mbalimnbali kikiwemo cha kereografu cha B 6.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Hoteli ya Doubletree by Hilton Zanzibar, Bw. Samuel(kulia)
Bond na Mkewe Jenny Bond wakibadilishana mawazo na mmoja wa majaji wa
tuzo za ZIFF 2014 Mykel Parish (aliyeipa mgongo kamera) kabla ya kuanza
kwa tuzo za ZIFF 2014.
Aidha
mwenyekiti huyo alisema kwamba Zuku itaendelea kuhakikisha inasaidia
kuinua kiwango cha uigizaji na utengenezaji sinema za Kiswahili kwa
kutambua kwamba filamu hizo ni sehemu ya uzalishaji wa fedha katika
taifa kupitia utamaduni.
Aidha
alisema pamoja na mamilioni ya shilingi walioyoahidi kutumbukiza katika
miaka 10 ni vyema taasisi nyingine hasa za umma kutambua uwapo wa
tamasha hilo ambalo likitumika vyema ni chanzo kikuu cha fedha kwa
serikali na watu wake.
Katika
utoaji wa tuzo ambao ulionekana nchi ya Afrika Kusini kufanya vyema,
mtendaji wa ZIFF Professor Martin Mhando alizungumza maana ya nchi za
majahazi na nini kinastahili kufanywa.
Mkurugenzi
Mkuu wa ZIFF, Profesa Martin Mhando akiwakaribisha wageni waalikwa
waliohudhuria usiku maalum wa tuzo za tamasha la 17 la ZIFF 2014
zilizofanyika mwishoni mwa juma.
Alisema
tamasha hilo halitabadili wajibu wake wa tangu awali wa,mkuchochea
mabadiliko miongoni mwa jamii na serikali hali ambayo inajenga jamii
yenye kuheshimu maendeleo na wajibu wa kila mmojawao.
Alisema
pamoja na kuwa na safari ndefu bado ZIFF ndio jukwaa lenye uhakika kwa
watengeneza sinemakatika bara la Afrika na kadhalika.
Katika utoaji tuzo,ZIFF ilialika zaidi ya watengeneza filamu 30 kutoka nchi mbalimbali.
ZIFF 2014 – AWARDS
SIGNIS AWARDS
SPECIAL MENTION
Shadow Tree
By BIja Viswa
(Tanzania)
EAST AFRICAN TALENT AWARD (1000 dollars)
Sticking Ribbons
by Bill Jones
(Kenya)
SIGNIS PRIZE
Espinho Da Rosa/ The Thorn Of The Rose
by Filipe Henriques
(Guine Bissao)
SEMBENE OUSMANE AWARDS
Umunthu,
by Mwizalero Nyirenda
(Malawi)
Body Games,
by Richard Pakleppa& Matthias Rohrig Assuncao
(Namibia / Brasil / South Africa)
SPECIAL MENTION
Welcome to Loliondo
by Morten West
(Denmark)
ZUKU BONGO MOVIES AWARDS
ZUKU PEOPLE CHOICE
Shikamoo Mzee
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Wananchi Group ambao ndio wadhamini wakuu wa tamasha
hilo, Bw. Richard Bell akizungumza na wageni waalikwa wakati utoaji tuzo
za ZIFF 2014 lililomalizika mwishoni mwa juma visiwani Zanzibar. Aidha
mwenyekiti huyo alisema kwamba Zuku itaendelea kuhakikisha inasaidia
kuinua kiwango cha uigizaji na utengenezaji sinema za Kiswahili kwa
kutambua kwamba filamu hizo ni sehemu ya uzalishaji wa fedha katika
taifa kupitia utamaduni na kutoa wito kwa wasanii wa Bongo Movie
kupeleka kazi zao kwa ajili ya kuonyeshwa kwenye chaneli za ving’amuzi
vya ZUKU na kujitangaza kimataifa kupitia ving’amuzi hivyo.
BEST ACTOR
Jackson Kabirigi
for Kisate and Nguvu ya Imani
BEST ACTRESS
Esha Buheti
for Mimi na Mungu wangu
BEST DIRECTOR
Issa Musa Cloud
for Shahada
BEST FEATURE FILM
Shahada
Issa Musa
ZIFF AWARDS
LIFETIME ACHIEVEMENT AWARD
Emerson Skeens
Founder of ZIFF
Awarded Posthumously
BEST DOCUMENTARY
Sobukwe: A Great Soul
Mickey Madoda Dube
(South Africa)
BEST ANIMATION
Khumba
Anthony Silverston
(SouthAfrica)
BEST SHORT FILM
Shadowtree
Mti Wakivuli / Biju Viswanath
(India / Tanzania)
BEST EAST AFRICAN TALENT
The King’s Virgin
Daniel Moss
(Tanzania/UK)
Mmoja
wa majaji wa tuzo za Signs kwenye tamasha la ZIFF 2014, Adinda Pamela
akitangaza washindi wa tuzo hizo. Katikati ni Mratibu wa Majaji wa tuzo
za ZIFF 2014, Fabrizio Colombo na kulia ni mmoja wa “ushers” akiwa
ameshikilia tuzo hiyo.
CHAIRMAN’s AWARD
Sodiq
Adeyemi Michael
(UK)
SPECIAL JURY AWARD
Julio Mesquith
Main Actor
The Thorn of the Rose
BEST FEATURE FILM (SILVER DHOW)
The Thorn of the Rose – Espinho da Rosa
by Filipe Henriques (Guinea Bissau)
BEST FEATURE FILM (GOLDEN DHOW)
Half of a Yellow Sun
Biyi Bandele (USA)
Mmoja
wa washindi wa tuzo za Signis alikuwa ni ADY de Batista malkia
wa Filamu ya Espinho da Rosa (the Thorn of the rose). Pichani ni ADY de
Batista akisindikizwa jukwaani kupokea tuzo na Meneja wake.
Mmoja wa majaji wa tuzo za Signis Adinda Pamela akimpongeza ADY de Batista baada ya kunyakua tuzo hizo.
ADY
de Batista akiongea kwa furaha kwenye usiku maalum wa tuzo za Signis
katika kusheherekea tamasha la 17 la ZIFF lililomalizika mwishoni mwa
wiki visiwani Zanzibar.
ADY de Batista akishuka jukwaani baada ya kupokea tuzo na Meneja wake.
Channel Coordinator wa ZUKU Swahili, Bilha Olimba akitangaza jina la mshindi wa tuzo za ZUKU PEOPLE’s CHOICE. Katikati ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Wananchi Group ambao ndio wadhamini wakuu wa tamasha hilo kupitia brand ya ZUKU, Bw. Richard Bell
Msanii
wa filamu nchini Shamsa Ford akielekea jukwaani kumchukulia msanii
mwezake Jacob Steven almaarufu kama JB alitwaa tuzo ya ZUKU PEOPLE’S
CHOICE kupitia filamu yake ya SHIKAMOO MZEE kwenye tamasha la 17 la ZIFF
lililomalizika mwishoni mwa juma visiwani Zanzibar.
Shamsa Ford akizungumza kwa niaba ya JB kabla ya kupokea tuzo hiyo.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Wananchi Group ambao ndio wadhamini wakuu wa tamasha
hilo kupitia brand ya ZUKU, Bw. Richard Bell akikabidhi tuzo ya ZUKU
PEOPLE’s CHOICE kupitia filamu ya SHIKAMOO MZEE ya mwigizaji Jacob
Steven almaarufu kama JB iliyopokelewa na msanii mwenzake Shamsa Ford.
Shamsa Ford akishukaa jukwaa kwa furaha isiyona kifani.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Wananchi Group ambao ndio wadhamini wakuu wa tamasha
hilo kupitia brand ya ZUKU, Bw. Richard Bell akimkabidhi tuzo mwigizaji
bora Jackson Laurent Kabirigi kupitia filamu ya “Kisate na Nguvu ya Imani” (wa pili kushoto) aliyeambatana na ndugu yake Feysal Arikardy (kushoto).
Mtayarishaji
wa filamu Swahiliwood, William Mtitu akielekea jukwaani kumpokelea tuzo
mwongozaji wa filamu Issa Mussa a.k.a Cloud 112 aliyetwaa tuzo ya
uongozaji bora kupitia filamu yake ya SHAHADA ndani ya tamasha la 17 la
ZIFF 2014.
Mtayarishaji wa filamu Swahiliwood, William Mtitu akimpokelea moja kati ya tuzo mbili za mwongozaji wa filamu ya SHAHADA Issa Mussa a.k.a Cloud 112 kutoka kwa Afisa
Mtendaji Mkuu wa Wananchi Group ambao ndio wadhamini wakuu wa tamasha
hilo kupitia brand ya ZUKU, Bw. Richard Bell. Tuzo ya pili ya Cloud 112
ilikuwa ni ya BEST FEATURE FILM kupitia filamu ya Shahada
LIFETIME ACHIEVEMENT AWARD iliende kwa Emerson Skeens Founder of ZIFF Awarded Posthumously.
Prof. Martin Mhando akikabidhi tuzo hiyo kwa mmoja wa wanafamilia wa Mwanzilishi wa tuzo za ZIFF marehemu Emerson Skeens.
Mwanafamilia wa Mwanzilishi
wa tuzo za ZIFF marehemu Emerson Skeens akitoa shukrani baada ya
kupokea hizo na kuwashukuru ZIFF kwa kutambua mchango wa ndugu yao.
Mmoja wa wageni waalikwa na familia yake wakifurahia kutolewa tuzo kwa Mwanzilishi wa ZIFF marehemu Emerson Skeens.
Mmoja wa majaji wa ZIFF, Wangeci Murage akikabidhi tuzo ya BEST FEATURE FILM (SILVER DHOW) kwa Malkia wa Filamu ya Espinho da Rosa (the Thorn of the rose) ADY de Batista.
ADY de Batista akipongezwa na jaji Mohammed Juma Ame mara baada ya kupokea tuzo hiyo ambayo ni ya pili.
Meneja wa ADY de Batista, Sholey Maqueta akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa ZIFF, Profesa Martin Mhando.
Mkurugenzi Mkuu wa ZIFF, Profesa Martin Mhando akimkabidhi CHAIRMAN’s AWARD kupitia documentary ya Sodiq iliyoandaliwa na Adeyemi Michael (UK).
ADY
de Batista akilia jukwaani wakati anaenda kupokea tuzo yake ya tatu
ndani ya tamasha la 17 la ZIFF lilitofikia tamati mwishoni mwa juma.
ADY
de Batista akiongea kwa furaha baada ya kupokea tuzo hiyo na
kuwashukuru waandaji wa tamasha la ZIFF pamoja na majaji waliofanikisha
zoezi zima la tuzo hizo.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Wananchi Group ambao ndio wadhamini wakuu wa tamasha
hilo kupitia brand ya ZUKU, Bw. Richard Bell akikabidhi tuzo hiyo kwa Malkia wa Filamu ya Espinho da Rosa (the Thorn of the rose) kutoka Guinea Bissau ADY de Batista.
Malkia
wa Filamu ya Espinho da Rosa (the Thorn of the rose) ya Filipe
Henriques kutoka Guinea Bissau ADY de Batista na Meneja wake wakishuka
jukwaani.
Meneja
wa Tamasha la ZIFF, Daniel Nyalusi (Dean), akitambulisha timu nzima
ilifanikisha kufana kwa tamasha hilo la 17 la ZIFF lililofikia ukingoni
mwishoni mwa juma.
Meneja
wa Tamasha la ZIFF, Daniel Nyalusi (Dean) akielezea kauli mbiu ya
tamasha la ZIFF 2015 litakalofanyika tarehe 18 hadi 6 July mwakani.
Burudani mbalimbali zilitolewa kwenye tamasha la 17 la filamu la kimataifa la Zanzibar (ZIFF).
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwamo waandishi wa habari waliohudhuria usiku maalum wa tuzo hizo.
Pichani juu na chini ni baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri wakati wa halfa ya utoaji wa tuzo hizo.
Baadhi ya wageni waalikwa wakiserebuka kwenye jukwaa la ZIFF.
Washindi
wa tuzo za ZIFF kwenye picha ya pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa
Wananchi Group ambao ndio wadhamini wakuu wa tamasha hilo kupitia brand
ya ZUKU, Bw. Richard Bell.
Mratibu wa Majaji wa tuzo za ZIFF 2014, Fabrizio Colombo kwenye picha ya pamoja na ADY de Batista.
Pichani juu na chini wageni mbalimbali wakipata picha za ukumbusho mara baada ya kupokea tuzo zao.
ADY de Batista akiwa kwenye picha ya pamoja na Msanii wa filamu nchini Vicent Kigosi
0 comments:
Post a Comment