CHAMA cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA), Visiwani Zanzibar, kimedai kusikitishwa na taarifa
za baadhi ya wabunge wake kurejea katika vikao vya Bunge Maalumu la
Katiba Mjini Dodoma kinyume na msimamo wa chama hicho pamoja na Umoja wa
Katiba ya Wananchi (UKAWA).
Taarifa iliyotolewa na
Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zanzibar, Bw. Hamad Yussuf, ilisema
kitendo hicho kimedhihirika pasipo shaka kuwa wabunge hao ambao ni
wajumbe wa Bunge hilo, wamekwenda kinyume na maadili ya chama na kanuni
za mwenendo wa maadili ya wabunge wa CHADEMA.
Alisema kwa mujibu wa
Katiba ya chama vifungu vya 2.0(a) na 3.0(b), vinazungumzia kushusha
hadhi ya chama mbele ya jamii ya Watanzania na wanachama wao nchi nzima.
"Kitendo hiki hakiwezi
kuvumilika na kamwe hatuwezi kulea utovu wa nidhamu uliopita
mipaka...wasaliti wa aina hii hawatakuwa na nafasi ndani ya chama chetu.
"Tumepokea kwa
masikitiko taarifa za baadhi ya wabunge wa CHADEMA ambao wanaounda
UKAWA, kurudi ndani katika shughuli za Bunge la Katiba kinyume na
maagizo ya vikao vya chama na makubaliano ya umoja huu," alisema.
Aliongeza kuwa, CHADEMA
Zanzibar wanaamini wajumbe hao watapatiwa nafasi ya kujieleza na
kuwasilisha utetezi wao ambapo vikao vya katiba vitakaa na kuhakikisha
nidhamu na maadili ya chama yanalindwa kwa gharama yoyote.
Chanzo:Majira
0 comments:
Post a Comment