Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
SERIKALI ya Sweden imetiliana saini mkataba wa sh. bilioni 11na
Serikali ya Zanzibar kwa ajili ya kuisaidia miradi ya maendeleo ikiwemo
nishati.
Mkataba huo ulisainiwa na Katibu mkuu wa Wizara ya Fedha, Khamisi
Mussa na afisa miradi ya maedeleo kutoka ubalozi wa Sweden, Malena Rosma
jana mjini Vuga visiwani hapa.
Akizungumza baada ya hafla hiyo, Mussa alisema Sweden imekua nchi
ambayo imekuwa ikisaidia Zanzibar katika miradi mbali mbali ikiwemo
sekta ya nishati, elimu na miundombinu pamoja na shughuli za uchaguzi.
Alisema mradi huo wa nguvu za umeme utakua wa miaka minne na
endelevu, lengo likiwa ni kuliwezesha Shirika la Umeme kufanya kazi
kiufanisi.
Kwa mujibu wa Mussa, Zeco inategemea kutumia umeme mbadala badala ya
kutumia ya ule unaotoka Tanzania bara kupitia cable za ndani ya bahari.
Aliishukuru serikali ya Sweden kwa misaada yao huku akisema kuwa
anaamini nchi hiyo itaisadia Zanzibar katika uchaguzi mkuu ujao.
Naye, Afisa wa miradi ya maendeleo kutoka ubalozi wa Sweeden, Malena
Rosma alisema lengo lao ni kuisadia Zeco ili iweze kufanya kazi zake
kiufanisi kwa ajili ya kuiletea maendeleo Zanzibar.
Kwa upande wake, Katibu mkuu wa Zeco, Alhalili Mirza alisema fedha
hizo zitatumika katika kupanga sera, kwani shirika halikwezi kuingia
kuanza kutumia umeme mbadala bila ya kujipanga.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment