Na Is-haka Omar, Zanzibar.
MGOMBEA
mteule wa Tiketi ya CCM jimbo la Dimani Unguja, Juma Ali Juma
amewashukuru na kuwapongezi viongozi wa ngazi zote za chama hicho kwa
jinsi walivyoendesha mchakato wa uteuzi wake.
Mteule
huyo ambae alitangazwa kati kati wa wiki hii baada ya kikao cha Kamati
Maalum ya halmashauri kuu ya CCM zanzibar alikuwa ni miongoni mwa makada
25 wa chama hicho waliojitokeza kuwania nafasi hiyo.
Akizungumza
na Gazeti hili jana mgombea huyo alisema anavipongeza vikao hivyo vya
CCM kwa kumuamini kumpa jukumu la kupeperusha bendera ya Chama hicho
katika Uchaguzi mdogo wa jimbo hilo na kuahidi kutekeleza wajibu huo
kikamilifu.
Alieleza
kuwa katika kutimiza wajibu huo kwa chama chake na wanancnhi kwa
ujumla, atahakikisha analinda, anaheshimu na kukiwakilisha vyema Chama
chake katika uchaguzi huo.
“Chama
Cha Mapinduzi kupitia watendaji, viongozi, makada na wachama wake wote
walioshirikiana kwa njia moja ama nyingine kuanzia hatua za awali mpaka
nateuliwa nawashukru sana kwa hekima na busara zao hakika sitowaangusha
popote nitakaposimama kunadi sera za chama na serikali iliyopo
madarakani.
Akizungumzia
ushindani katika mchakato wa kumpata mgombea ndani ya chama, Juma
alisema ulikuwa mkubwa uliotawaliwa na demokrasia, uhuru na maamuzi
yaliyojaa busara.
“Ushindani
uliokuwepo katika uchaguzi wa ndani ya chama ni kipimo tosha cha
kunifanya niamini kuwa walioniteuwa wamejiridhisha kuwa nafaa kuvaa
viatua vya alikuwa Mbunge wa jimbo hili marehemu Tahir (Hafidh Ali).”,
alieleza Juma.
Sambamba
na hayo mteule huyo aliweka wazi baadhi ya mambo atakayoyapigania ikiwa
ni pamoja na kuhakikisha anasimamia utekelezwaji wa ilani ya uchaguzi
ya CCM ya mwaka 2015/2020 kwa manufaa ya wananchi wa jimbo hilo bila ya
ubaguzi.
Jumla
ya vyama viwili Zanzibar vimetangaza nia ya kushiriki katika uchaguzi
huo ambavyo ni Chama Cha Wananchi (CUF) na CCM ambavyo vimekamilisha
mchakato wa kumpata mgombea katika uchaguzi huo unaofanyika baada ya
kifo cha aliekuwa Mbunge wa jimbo hilo marehemu Hafidh Ali Tahiri
aliyefariki mwezi uliopita mjini Dodoma.
MWISHO.

0 comments:
Post a Comment