MAKAMU
Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi (BLM), Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein, kesho tarehe 15/12/2016
anatarajia kukiongoza Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM
Taifa.
Kwa
mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo na Katibu wa
Kamati Maalum ya NEC Zanzibar - Idara ya Itikadi na Uenezi, Mhe. Waride
Bakar Jabu, amesema kikao hicho cha kawaida cha siku moja kitafanyika
Afisi Kuu ya CCM, Kisiwandui kuanzia saa 4:00 asubuhi.
Amesema
kikao pamoja na mambo mengine, kitapokea na kujadili Mapendekezo ya
wanachama wa CCM wanaoomba kuteuliwa kugombea nafasi ya Ubunge katika
Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Dimani na kuongeza kuwa maandalizi yote
yamekamilika.
Aidha,
Katibu Waride amesema kikao hicho kilitanguliwa na Kikao cha
Sekretarieti ya Kamati Maalum ya NEC, kilichokutana tarehe 14 Novemba,
mwaka huu, chini ya Mwenyekiti wake Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar
Mhe. Vuai Ali Vuai, kwa lengo la kuandaa Agenda za kikao hicho.
“KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI”
……………..
Waride Bakar Jabu
Katibu wa Kamati Maalum ya NEC
Idara ya Itikadi na Uenezi - CCM
ZANZIBAR.
14/12/2016

0 comments:
Post a Comment