Na Is-haka Omar , Zanzibar.
CHAMA
Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimewaonya baadhi ya viongozi na wanachama
wanaowashutumu na kuwadhalilisha viongozi wenzao katika vyombo vya
habari na hadharani kinyume na utaratibu wa taasisi hiyo.
Onyo
hilo limetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai
wakati akitoa mada ya Muelekeo wa Uchaguzi Mkuu wa CCM mwaka 2017/2022
katika mafunzo maalum ya siku Moja ya viongozi na watendaji wa chama
hicho ngazi za matawi, wadi na majimbo ya Wilaya ya Kaskazini “B” Unguja
kichama.
Alisema
viongozi na wanachama wenye tabia hiyo ndani ya CCM hawawezi kuvumiliwa
na watachukuliwa hatua za kinidhamu kupitia vikao vya maadili vya chama
hicho endapo watathibitika kukutwa na hatia ya kuwajibika.
Alifafanua
kwamba Chama hicho kikiwa ndio kinara wa Demokrasia katika mfumo wa
vyama vingi Tanzania, utamaduni wa kukosoana, kuelekezana , wajibishana
na kufanya maamuzi mazito kwa baadhi ya mambo yasiyokwenda sawa
kimaadili na kiuongozi upo lakini kwa kufuata utaratibu wa vikao rasmi
vya kikanuni ndani ya chama na sio hadharani.
“
Kuna tabia imezuka kwa baadhi ya viongozi na wanachama ndani ya CCM
Zanzibar wamekuwa wababe kiasi cha kuwashutumu viongozi wenzao shutuma
nzito, tena hadharani na kupitia vyombo vya Habari, wakati kuna fursa
pana ya vikao vya chama ambayo ndio sehemu pekee ya kuelekezana kwa
lengo la kupata ufumbuzi wa tatizo.
Tabia
hiyo hatuwezi kuivumilia lazima tukate mizizi mapema kabla haijakomaa
na kukiangamiza chama chetu, na wote wanaohusika na tuhuma hizo kwa sasa
tunawachunguza na kuwafuatilia kwa kina ili kujiridhisha na yeyote
atakayekutwa na hatia vikao vya Maadili vya chama vitachukua hatua
stahiki bila ya kumuonea mtu yeyote.” Alieleza Vuai huku akiwataka
wanaofanya vitendo hivyo kuacha mara moja.
Vuai
alisisitiza kauli yake na kuahidi kuwa Chama hicho Zanzibar
hakitomvumilia kiongozi yeyote anayevunja maadili ya uongozi kwa
makusudi badala yake kitamshughulikia bila kujali cheo na umaarufu wake
kisiasa.
Aliziagiza
Kamati za Maadili kwa ngazi mbali mbali katika maeneo yaliyozuka
migogoro hiyo kuanza mara moja kutekeleza wajibu wao wa kuwaita viongozi
hao katika vikao vya kikanuni ili kusuluhisha na ikishindikana wafuate
utaratibu na kuwapeleka katika ngazi zingine za maamuzi.
Alitoa
wito kwa viongozi na watendaji wa Chama na jumuiya zake pamoja na
wanachama kwa ujumla kusoma Ibara ya 18 ya Katiba ya CCM ya mwaka 1977
toleo la mwaka 2012 inayoelekeza kuwa ni Mwiko kwa kiongozi “ Kutumia
madaraka aliyopewa ama kwa ajili ya manufaa yake binafsi au kwa
upendeleo , au kwa namna yoyote ambayo ni kinyume cha lengo
lililokusudiwa madaraka hayo”., alinukuu kifungu hicho Vuai.
Naibu
Katibu Mkuu huyo akizungumzia mulekeo wa CCM aliwataka viongozi,
watendaji na wafuasi wa Chama hicho kujiandaa kikamilifu kukabiliana na
mabadiliko ya muundo mpya wa Chama na Jumuiya zake.
Alisema
mabadiliko hayo yanatokana na kikao Cha Halmashauri Kuu ya Taifa
kilichokaa Disemba 13 mwaka 2016, kufikia maamuzi ya kupitisha
mapendekezo ya Kamati Kuu ya kufanya mabadiliko ya muundo wa Chama
hicho.
Vuai
alieleza kuwa lengo la kufanyika kwa mabadiliko ya muundo wa chama ni
kuimarisha uhai wa taasisi hiyo kiutendaji na kiuongozi ili iweze
kufanya kazi zake kwa ufanisi kulingana na wakati uliopo sasa katika
ushindani wa kisiasa.
Hata
hivyo aliyataja baadhi ya mapendekezo yaliyofikiwa katika Kikao hicho
kuwa ni pamoja na kupunguza idadi ya wajumbe na vikao ambayo kwa sasa ni
kubwa na inafanya chama hicho kishindwe kutekeleza vizuri baadhi ya
majukumu yake.
“
Wajumbe tulitafakari kwa kina muelekezo wa CCM, mienendo ya kiutendaji
ya watumishi na viongozi pamoja na mahitaji halisi ya wanachama wetu
tukaona kuna haja ya kufanyika mabadiliko ili tutabane matumizi kwa
kupunguza baadhi ya gharama zisizokuwa za msingi ndani ya chama.
Ili
chama chetu kiendelee kuwa mwalimu wa Demokrasia ndani na nje ya
Tanzania lazima wanachama wote tuwe wamoja na wenye mshikamano katika
kuunga mkono juhudi za kuleta mabadiliko yenye ufanisi kiutendaji ndani
ya chama hicho.”, alielza Vuai.
Naibu
Katibu Mkuu huyo alifafanua baadhi ya mapendekezo yaliyotolewa na kikao
hicho kuwa yaliamua kupunguza Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa
kutoka 388 na kupendekezwa wawe 158 kutoka Tanzania bara na Zanzibar.
Kwa
upande wa ngazi ya Kamati Kuu walipendekezwa wawe wajumbe 24 badala 34
ambapo kati ya hao wajumbe watatu watachaguliwa na Halmashauri Kuu
kutoka Tanzania bara na watatu wengine watachaguliwa na Halmashauri kuu
ya Zanzibar.
Alisema
maandalizi ya kufanyika kwa muundo huo ndani ya Chama yalianza
zamani kwani yalikuwa yafanyike mwaka 2012, na kuhairishwa kutokana na
sababu zisizoweza kuepukika.
Alisema
baada ya kuhairishwa kufanyika kwa muundo huo chama kiliendelea
kujipanga kwa kuwashirikisha wataalamu wa masuala ya kisiasa, kutoka
Vyuo ili watathimini na kutoa ushauri wa kitaalamu utakaozaa muundo
unaokidhi mahitaji ya wanachama.
Alibainisha
kuwa Mapendekezo hayo yatapelekea kufanyika kwa mabadiliko ya Katiba ya
Chama na kanuzi za jumuiya na chama, na kuongeza kuwa vyeo ambavyo
havitokuwemo katika Katiba hiyo havitoruhusiwa ndani ya Chama jumuiya.
Vuai
aliwataka viongozi wanaohusika na vikao vya kuchuja waombaji wa nafasi
za uongozi kufuata maadili ya kikanuni kwa kuhakikisha, muombaji
ametimiza masharti ya uanachama kwa mujibu wa ibara ya 8 ya Katiba ya
CCM.
Alitoa
angalizo kwa wanachama wa chama hicho kuhakikisha wanachagua viongozi
wenye uwezo, waadilifu na waumini wa kweli wa CCM watakaoweza kusimamia
maslahi ya Chama kwa vitendo.
“
Tutumie vizuri fursa hii ya uchaguzi kwani ndio sehemu pekee ya kupata
timu imara ya kuongoza jahazi la CCM kwa ufanisi na mafanikio makubwa
kwa miaka mitano ijayo.
Pia
ngazi husika hasa Kamati za siasa kwa ngazi mbali mbali lazima mtoe
taarifa na matangazo mapema kwa wanachama ili waweze kujitokeza kwa
wingi kuwania nafasi za uongozi kwani ni haki ya kikatiba kwa kila
mwanachama kuchagua na kuchaguliwa ’’ Alisisitiza kiongozi huyo.
Aidha
aliwataka wabunge, wawakilishi na madiwani kutengeneza mazingira rafiki
ya upatikanaji kwa urahisi fursa za Mikopo na mafunzo ya Ujasiriamali
kutoka katika taasisi zinazozihusika na masuala ili ziweze kuwasaidia
vijana ambao hawapo katika mfumo rasmi wa ajira na waweze kujiajiri
wenyewe.
Nao
Washiriki wa Mafunzo hayo waliwashauri viongozi na Watumishi wa CCM na
Jumuiya zake wa ngazi za Juu kuonyesha mfano wa kiutendaji ili viongozi
na wanachama wa ngazi za chini waweze kufuata nyayo hizo kwa vitendo.
Walisema
licha ya Mkoa huo kuwa na fursa ya Hoteli nyingi za Kitalii na
rasilimali ya bahari bado kundi la vijana wanakabiliwa na tatizo la
upungufu wa ajira, jambo linalotakiwa kutafutiwa ufumbuzi wa kudumu na
serikali kwa kushirikiana na Chama.
Mafunzo
hayo ya siku moja yamewashirikisha jumla ya viongozi na watendaji 487
wa chama na jumuiya wa ngazi za matawi, wadi na majimbo ya Wilaya ya
Kaskazini “B” kichama.
0 comments:
Post a Comment