Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Baraza la Wazee wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar kwa niaba ya wazee wote
wa Chama hicho linampongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi, Ambae pia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali
Mohammed Shein kwa kutimiza ahadi yake ya kuinua kiwango cha chini cha
Mishahara 100% kwa watumishi wa Umma, hatua iliyoanzia mwezi wa April,
2017.
Pia wamemuomba Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kuendelea kusimamia kwa umakini mambo yafuatayo:-
1.Kuwabana wasiolipakodi hasa baadhi ya wafanyabiashara wenye tabia za ukwepaji wa kodi hizo.
2. Kusimamia Bodi zinazoshughulikia masuala ya upandaji wa bei za bidhaa
ili kuzuwia mfumko wa bei hizo zinazopanda bila ya kuzingatia kipato
cha wananchi.
3. Pia, Afanye tathmini zitakazosaidia kusimamia rasli mali za Zanzibar
ili zitumike kwa uangalifu zaidi kwa kuwanufaisha wananchi wote.
Aidha, tumefurahishwa na tukio la kupunguza kodi ya mapato kutoka
kiwango cha asilimia 13% hadi asilimia 9% Lakini pia kusimamia na
kuwajibisha watendaji wasio waaminifu kwa Serikali.
Pamoja na pongezi zetu wazee tunatoa nasaha kwa watumishi wa Umma kwa
kuwaomba wafanye kazi kwa bidii na uadilifu. Mwisho sisi wazee
tunawatakia mema wafanyakazi wa SMZ katika maisha yao na tunamuombea
Mhe. Rais Dk. Ali Mohamed Shein na familia yake maisha mema, afya bora
na mafanikio makubwa.
AHSANTENI SANA
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
MAPINDUZI DAIMA
CCM OYEE!
(KHADIJA JABIR)
MWENYEKITI WA BARAZA LA WAZEE WA CCM
ZANZIBAR
02/05/2017
Home »
» WAZEE WA CCM Z'BAR WATOA WAMPONGEZA DR.SHEIN NA KUTOA MAPENDEKEZO MAZITO.
0 comments:
Post a Comment