Mjumbe wa kamati ya Siasa ya CCM Wilaya ya Kaskazini B Mama Asha
Suleiman Iddi akisisitiza jambo wakati akiufungua Mkutano wa Umoja wa
Wapanda Mapiki Piki wa Wilaya hiyo hapo Ukumbi wa CCM Jimbo la Kitope
uliopo Kinduni.
Mjumbe wa Kamati wa Siasa ya CCM Wilaya ya Kaskazini B Mama Asha
Suleiman Iddi akimkabidhi mchango wa shilingi Laki Tatu { 300,000/- }
Mwenyekiti wa Umoja wa Wapanda Mapiki Piki Wilaya ya Kaskazini B nd.
Mosi Ame Mosi.
Mchango huo ni kwa ajili ya kusaidia utunishaji wa mfuko wa Umoja huo
ambao ni muhimili muhimu katika uhamasishaji ndani ya Chama Cha
Mapinduzi.
Wajumbe wa Umoja wa Wapanda Mapiki Piki wa Wilaya ya Kaskazini “B”
wakifuatilia kwa makini hotuba ya ufunguzi wa Mkutano wao iliyotolewa na
Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya hiyo ambaye pia ni Mke wa Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi hayupo pichani.
Ufunguzi huo umefanyika katika Ofisi ya CCM ya Jimbo la Kitope iliyopo
Kinduni Wilaya ya Kaskazini B.
wakifuatilia kwa makini hotuba ya ufunguzi wa Mkutano wao iliyotolewa na
Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya hiyo ambaye pia ni Mke wa Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi hayupo pichani.
Ufunguzi huo umefanyika katika Ofisi ya CCM ya Jimbo la Kitope iliyopo
Kinduni Wilaya ya Kaskazini B.
---
Vijana ndani ya Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake wamesisitizwa
kuendelea kutunza amani iliyopo na kujiepuka na shari inayoweza kuzaa
balaa na hatimae kuzagaa kwa maafa Nchini.
Sisitizo hilo limetolewa na Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM ya Wilaya
ya Kaskazini B ambaye pia ni Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Mama Asha Suleiman Iddi wakati akiufungua Mkutano Mkuu wa Umoja wa
Wapanda Mapiki Pili wa Wilaya hiyo hapo Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya
CCM Jimbo la Kitope uliopo Kinduni.
Mama Asha amesema Vijana hao wanapaswa kuwa waangalifu zaidi kutokana na
vitendo vinavyoashiria fujo ambavyo huonekana kukumba zaidi kundi
kubwa la Vijana.
Amesema suala la utunzaji wa Amani linamuhusu kila Mwana Jamii kwani
hata Dini zote pamoja na Madhehebu mbali mbali zimekuwa zikihubiri na
kuhimiza suala la utunzwaji wa Amani.
Akizungumzia suala la Uchaguzi Mama Asha aliwahimiza Wajumbe wa Mkutano
huo kuhakikisha Wanawachaguwa Viongozi Makini watakaokuwa Mahiri kwenye
uendelezaji wa Ushindi wa Chama chao Katika Uchaguzi ujao.
Alisema Tabia ya Baadhi ya Watu kuchagua Viongozi kwa misingi ya Ukabila
na kujuana imepelekea kukitia doa kubwa Chama Hicho ambacho ndio
kimbilio la Wanyonge Nchini.
“ Ukweli tabia hii mbaya sana inakera na inafaa kuepukwa mara moja kwa
vile inapunguza kwa kiasi kikubwa nguvu ya Chama ”. Alisisitiza Mama
Asha.
Mama Asha aliwakumbusha Vijana hao kuendelea kuyatetea Mapinduzi ya
Zanzibar ya Mwaka 1964 ambayo yalileta faraja kwa Wananchi walio wengi
hapa Zanzibar.
Alisema Vijana wanapaswa kuwa makini katika kutetea Viongozi wao
kutokana na tabia ya baadhi ya watu kuendeleza tabia ya kuhubiri Matusi
hadharani hana sababu dhidi ya Viongozi hao.
Katika kuunga Mkono juhudi za kuendeleza Umoja huo wa Wapanda Mapiki
Piki wa Wilaya ya Kaskazini B Mama Asha amechangia jumla ya Shilingi
Laki Tatu Taslimu { 300,000/- } kusaidia kutunisha Mfuko wa Umoja huo.
Katika Risala yao iliyosomwa na Katibu Msaidizi wa Umoja huo Nd. Ame
Pandu Kombo Vijana hao wameahidi kuendelea kuhamasisha Wananchi pamoja
na Wanachama katika kuunga mkono Sera za Chama Tawala ambacho ndio
kimbilio la Wananchi walio wengi Nchini.
Nd. Ame alisema Umoja wao licha ya kazi kubwa wanayoendelea kuitekeleza
lakini bado wanakabiliwa na Changa moto mbali mbali zinazokwamisha
kutekeleza majukumu yao.
Alizitaja Changa moto hizo kuwa ni pamoja na ufinyu wa sare wakati
wanapokuwa katika shughuli zao za uhamasishajipamoja na Mtaji mdogo wa
Umoja wao unaopelekea kushindwa pia kufungua Akaunti Benki.
Mapema akimkaribisha Mgeni Rasmi kufungua Mkutano huo, Mwenyekiti wa
Umoja wa Wapanda Mapiki Piki Wilaya ya Kaskazini B Nd. Mosi Ame Mosi
aliwatahadharisha Vijana hao kuwa mbali na Makundi ya sasa
yanayopandikizwa cheche za kuchafua amani ya Nchi katika maeneo mbali
mbali hapa Nchini.
Na
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu Wa Pili Wa Rais Zanzibar
0 comments:
Post a Comment