Na Mohammed Mhina, Zanzibar
SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imeainisha mpango wa matumizi ya Sh bilioni 14.8, zilizotolewa kama msaada na Serikali ya China. Akizungumza mjini hapa jana, Waziri wa Fedha wa SMZ, Omar Yusuf Mzee, alisema kipaumbele cha kwanza katika fedha hizo itakuwa ni kuboresha huduma za afya, elimu na miundombinu ya maji pamoja na uwekaji wa taa za sola katika baadhi ya barabara za mji wa Zanzibar.
Akizungumzia huduma za afya, alisema sehemu ya fedha hizo zitasaidia upanuzi na ujenzi wa Hospitali ya Mkoani, Kisiwani Pemba na kuifanya kuwa ya rufaa.
Alisema taratibu zote za ujenzi wa hospitali hiyo zimekamilika na ujenzi huo utakapokamilika hakutakuwa na haja tena ya wagonjwa mahututi kuletwa katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja, kwa vile itakuwa na kila aina ya vifaa na dawa za tiba.
Alisema fedha hizo pia zitasaidia kuwasomesha wataalamu wa afya, walimu wa masomo ya sayansi na kuboresha Shule ya Msingi ya Mwanakwerekwe kwa kuongeza ujenzi wa vyumba 12 vya madarasa.
Alisema fedha hizo pia zitasaidia kuweka taa za sola katika baadhi ya barabara za mji wa Zanzibar na kuboresha miundombinu ya maji mijini na vijijini.
Alisema visima virefu na vifupi vitachimbwa kuongeza rasilimali ya maji katika maeneo mbalimbali ya visiwa vya Unguja na Pemba na kupunguza adha ya upatikanaji wa maji mijini na vijijini.
Alisema fedha hizo zitasaidia kusomesha wataalamu, wakiwamo madaktari na wataalamu wa fani mbalimbali.
Aidha, alisema pia kuna suala la ununuzi wa meli ya Serikali itakayokidhi huduma za usafirishaji wa abiria na mizigo kati ya Unguja na Pemba.
Alisema wanaendelea na mchakato wa ukusanyaji wa fedha Sh bilioni 17.6 kutoka katika vifungu 19 vya bajeti ya ndani kupitia katika wizara mbalimbali kwa ajili ya kununulia meli itakayokidhi mahitaji ya usafiri wa abiria na mizigo.
Alisema meli hiyo itakayogharimu zaidi ya Dola milioni 12 za Kimarekani, itatengenezwa kwa muda wa miezi 18 na itasimamiwa na Kampuni ya Rowdies ya Uingereza.
Alisema kinachofanyika sasa ni kuboresha michoro ya muundo wa meli hiyo kwa ajili ya kukidhi vigezo na viwango vya usafiri.
Alisema Serikali ikiendelea na mchakato huo, kuna juhudi nyingine zinazochukuliwa na baadhi ya kampuni za usafirishaji majini, ikiwamo ya Azam Marine za kutaka kuingiza nchini meli nyingine kubwa kusaidia kupunguza adha ya usafiri wa abiria na mizigo.

Chanzo: Mtanzania
0 comments:
Post a Comment