Home » » WAFANYABISHARA WETE WAKOPESHWA MILIONI 350

WAFANYABISHARA WETE WAKOPESHWA MILIONI 350

Mwandishi wetu, Pemba-Zanzibar Yetu

Jumla ya mikopo 104 yenye thamani ya shilingi milioni 350 imetolewa kwa wanachama wa MUWAPE Saccos iliyoko mtemeni Wilaya ya Wete ili wajiendeleze kibiashara na kuweza kupambana na hali ya umaskini wa kipato katika familia zao .

akizungumza na mwandishi wa habari hizi huko ofisini kwake mtemani wete mwenyekiti wa saccos hiyo salim khamis salim amesema kuwa mikopo hiyo imelenga kuwaimarisha kiuchumi wanachama wa saccos hiyo na hivyo kuunga mkono mpango wa Taifa wa kupunguza na umaskini MKUZA .

amesema kuwa wanachama wa saccos hiyo wengi wao wameitikia wito wa serikali yao wa kuwataka kutotegemea ajira kutoka serikalini , na kwamba MUWAPE saccos imekuwa ni mkombozi wa wanyonge hasa wananchi wenye kipato cha chini na wanaoishi vijijini .

aidha amesema katika kuona kwamba mikopo hiyo inawanufaisha wananchama wake , uongozi wa saccos umeunda kamati ya ufuatiliaji ambapo kamati hiyo imekuwa ikifanya tathmini juu ya mtaji wa mkopaji kulingana na kiwango cha fedha anachotaka kukopa  kabla hajapatiwa mkopo .

Mwenyekiti huyo amesema lengo la baadaye la saccos hiyo ni kufungua benki ya jamii ambayo itakuwa ikitoa mikopo kwa wananchama yenye masharti nafuu ambapo kila mwanachama atamudu kukopo na kulipa kwa wakati .

akizungumzia suala la ujereshaji wa mikopo  mshika fedha wa saccos hiyo fatma suleiman khatib amesema wanachama wanatambua umuhimu wa kurejesha mikopo kwa wakati , kutokana na elimu waliyopatiwa na uongozi .

muwape saccos  ni muungano wa kampuni 19 za wajasiriamali  wa Pemba na imeanzishwa mwaka  2010  ikiwa na wanachama  39 na hadi kufikia septemba 30 mwaka huu  ina jumla ya wanachama 250 .

Blogzamikoa

0 comments:

Post a Comment

 
Support by Blogs za Mikoa Tanzania
Copyright © 2012. Zanzibar Yetu - All Rights Reserved
Designed by by Blogs za Miikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa