Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
- Wananchi wa Zanzibar wasema serikali mbili zatosha
- Wachukizwa na wanasiasa wanafiki wanaopindisha pindisha maneno
- Vijana wa CCM kutovumilia wanasiasa wanaokashifu waasisi wa Taifa letu
- Wasema wamechoshwa na matendo ya Viongozi wa Vyama vya Upinzani wataka muswada wa kuujadili Serikali wa Umoja wa kitaifa wataka ufutwe kwani hauna faida kwa maendeleo yao .
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Zanzibar na
kuwaambia CCM itasimamia haki za Wazanzibar na kuhakikisha Muungano
unadumu na Mapinduzi ya Zanzibar yanaenziwa .
Wananchi wakionyesha ishara ya Serikali mbili kwenye mkutano wa CCM kwenye viwanja vya Kibanda Maiti, Unguja Zanzibar.
Naibu
Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na watoto akionyesha ishara ya
serikali mbili wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja
vya kibanda maiti na kuwataka wanawake wote wa Zanzibar kuungana katika
kusimamia Muungano wa Tanzania.
Mbili zatosha.
Kila mtu alionyesha mapenzi yake kwa CCM.
Wakazi wa Zanzibar hawakujali mvua iliyokuwa inanyesha kwenye mkutano wa CCM Kibanda Maiti Zanzibar
Mama
Fatma Karume akihutubia wakazi wa Unguja na kuwaambia kuwa waasisi wetu
waliweka uzio wa kutulinda na kudumisha umoja na undugu wetu na kusema
uzio huo ni Muungano wetu.
Mjumbe
wa Kamati Kuu ya CCM na Mbunge wa BundaStephen Wassira akihutubia
wananchi wa Zanzibar ambapo alisema UKAWA wanatakiwa kuelewa misingi ya
Muungano kwanza kisha waje na hoja .
Mbunge
wa Songea Mjini Dk Emmanuel Nchimbi akihutubia wakazi wa Unguja kwenye
mkutano wa hadhara uliofanyika Kibanda Maiti na kuwataka wananchi hao
kuwa makini na viongozi wanaogeuza maneno huku akitolea mfano kutoka
kwenye kitabu cha Maalim Seif.
Katibu wa NEC Oganizeshen Dk. Mohamed Seif Khatibu akihutubia wakazi wa Unguja kwenye mkutano wa hadhara Kibanda maiti .
Sehemu
ya Umati uliohudhuria mkutano wa hadhara ambao ulihutubiwa na Viongozi
mbali mbali wa CCM wakiongozwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman
Kinana.
0 comments:
Post a Comment