Home » » UVCCM YATAKA MOYO ATOSWE CCM

UVCCM YATAKA MOYO ATOSWE CCM

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Hassan Nassor Moyo
 
Jumuiya ya Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) imesema  imechoshwa na vitendo vya muasisi wa chama hicho, Hassan Nassor Moyo, kwa madai ya kukisaliti na kukidhoofisha chama hicho.
 Akizungumza na waandishi wa habari  jana, Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar, Shaka Hamdu Shaka, aliwataka viongozi wakuu wa CCM kuchukua hatua za  kinidhamu na  kumnyang’anya kadi ya uanachama muasisi huyo.

Moyo ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maridhiano ambayo ilihusika wakati wa kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) na ni mtetezi wa muundo wa serikali tatu.

 Shaka alisema kwa muda mrefu Mzee Moyo  amekuwa akikihujumu CCM bila ya kuchukuliwa hatua za kinidhamu, na kwamba hali hiyo  linakidhoofisha chama hicho na kukivunjia hadhi mbele ya wananchi, hivyo wakati umefika kwa muasisi huyo kufukuzwa CCM.

‘CCM kina mtaji wa wanachama, viongozi na waasisi wengi, si maskini, heri wabaki wachache kuliko kuendelea kubaki na wanachama wasaliti na wakorofi,” lisema Shaka.

 Shaka alisema Moyo amekuwa akitumia mwavuli wa uanachama wa CCM kukivuruga na kukisaliti chama hicho kupitia Kamati ya Maridhiano ambayo alisema haikuundwa kwa mujibu wa sheria wala Katiba ya Zanzibar na kwamba Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, alishasema  hadharani kwamba kamati hiyo haitambui.

“Hii ni kamati ya upekepeke inayomzunguka na kumyumbisha  Rais Shein, haikuundwa kisheria, haina hadidu za rejea, haifahamiki kazi zake, kwanini ipande jukwaa la CUF na kuliogopa la CCM?” alihoji Shaka.

Mzee Moyo alipoulizwa, alisema hashughulishwi na maneno yao na kuwa ni mwanachama wa CCM, ana haki ya kutoa maoni na anaona Serikali tatu ndizo zinazofaa.
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

Post a Comment

 
Support by Blogs za Mikoa Tanzania
Copyright © 2012. Zanzibar Yetu - All Rights Reserved
Designed by by Blogs za Miikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa