Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MAKACHERO wa Jeshi la
Polisi Zanzibar,wamefanikiwa kumtia mbaroni mmoja wa washukiwa wa
matukio ya tindikali visiwani hapa, Alawi Mohammed Silima (25), mkazi wa
Fuoni Melinne nje kidogo ya mji wa Zanzibar.
Ofisa Habari Mkuu wa
Jeshi la Polisi Zanzibar Inspekta Mohammed Mhina, alisema mtuhumiwa
anahusishwa na tukio la kummwagia tindikali Sheha wa Shehia ya Tomondo
mjini Zanzibar, Mohammed Omar Saidi Kidevu kabla ya kutoweka.
Inspekta Mhina alisema,
mtuhumiwa huyo ambaye kwa muda mrefu alikuwa akisakwa na Polisi kwa
kuhusiana na tukio hilo, alikamatwa juzi usiku akiwa mafichoni katika
eneo la Fuoni baada ya taarifa za kiintelijensia kubaini kuwepo kwake.
Bado Makachero hao
wanaendelea kumhoji mtuhumiwa huyo kwa lengo la kubaini mtandao mzima wa
matukio mbalimbali ya kiwemo ya tindikali yaliyotokea siku za nyuma
visiwani humo.
Kukamatwa kwa mtuhumiwa
huyo kunatokana na taarifa za siri za raia wema ambapo Jeshi la Polisi
lilikuwa likiendelea na upelelezi wa chini kwa chini ili kumbaini
mtuhumiwa na mahali alipojificha.
Tukio la kumwagiwa
tindikali kwa Sheha huyo, lilitokea saa 2.45 usiku Mei 22, mwaka jana,
wakati alipokuwa akirudi nyumbani akitoka kuchota maji nyumba jirani
Chanzo;Majira
0 comments:
Post a Comment