Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiagana
na Mwenyekiti wa CUF Wilaya ya Magharibi Bi. Raisa Abdallah baada ya
kumaliza ziara yake ya kutembelea wagonjwa katika Wilaya hiyo.
Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad,
akiwapungua mkono wananchi katika eneo la Saateni wakati akiendelea na
ziara yake ya kuwatembelea wagonjwa katika Mkoa wa Mjini Magharibi.
Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akimfariji
kijana Hamza Omar Juma, anayesumbuliwa na matatizo ya moyo katika eneo
la Mtoni Kidatu.
Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad,
akiwapungua mkono wananchi, wakati akiendelea na ziara yake ya
kuwatembelea wagonjwa katika Mkoa wa Mjini Magharibi
Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwa
katika mitaa ya Muembe Makumbi kuendelea na ziara yake ya kuwatembelea
wagonjwa katika Mkoa wa Mjini Magharibi. (Picha na Salmin Said, OMKR).
Na Hassan Hamad OMKR
Wagonjwa wapatao 35 walioko majumbani wamepatiwa huduma na ushauri wa kiafya katika Wilaya sita za Unguja.
Hatua hiyo imefikiwa kufuatia ziara ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa
Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, ya kuwatembelea na kuwafariji
wagonjwa na wafiwa katika maeneo mbali mbali ya Zanzibar mjini na
vijijini.
Katika ziara hiyo, pamoja na mambo mengine wagonjwa wamekuwa wakipatiwa
baadhi ya dawa muhimu kulingana na maradhi yanayowakabili, sambamba na
kupatiwa ushauri wa kitaalamu kuhusiana na matatizo yao.
Mhe. Maalim Seif amekamilisha ziara yake ya siku tatu ya kutembelea
wagonjwa kwa upande wa Unguja iliyoanzia Mkoa wa Kaskazini Unguja na
kumalizikia Mkoa wa Mjini Magharibi.
Makamu wa Kwanza wa Rais anatarajiwa kufanya ziara kama hiyo katika Mikoa miwili ya Pemba kuanzia wiki ijayo.
0 comments:
Post a Comment