Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein jana aliwaapisha mawaziri, wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya waliopewa majukumu mapya.
Walioapishwa ni Dk Sira Ubwa Mamboya kuwa Waziri wa Kilimo na Maliasili, Juma Duni Haji kuwa Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano na Rashid Seif Suleiman, kuwa Waziri wa Afya.
Wengine walioapishwa katika hafla hiyo ni Mahmoud Thabit Kombo kuwa Naibu Waziri wa Afya na Meja mstaafu Juma Kassim Tindwa, kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Omar Khamis Othman aliapishwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Mwanajuma Majid Abdulla kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Ayub Mohamed Mahmoud kuwa Mkuu wa Wilaya ya Magharibi na Hanuna Masoud Ibrahim, kuwa Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Pemba.
Hafla hiyo ilifanyika Ikulu mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali, akiwemo Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharif Hamad.
Viongozi wengine waliohudhuria ni Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Abdalla Mwinyi Khamis, Mufti wa Zanzibar Shekhe Saleh Omar Kabih na Kadhi Mkuu wa Zanzibar, Shekhe Khamis Haji.
Pia alikuwepo Meya wa Manispaa ya Zanzibar, Khatib Abrahman Khatib, washauri wa Rais wa Zanzibar na viongozi wengine wa Serikali.
Kabla ya Uteuzi huo, Dk Mamboya alikuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Duni alikuwa Waziri wa Afya na Suleiman alikuwa Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano.
Meja mstaafu Tindwa alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mwajuma alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Pemba na Omar alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Wete.
Mahmoud alikuwa Ofisa Tawala Mkoa wa Mjini Magharibi na Hanuna alikuwa Ofisa Tawala Mkoa wa Kusini Pemba.
Chanzo;Habari Leo
0 comments:
Post a Comment