Home » » MSAFARA WA MAALIM SEIF WAPATA AJALI MISUNGWI

MSAFARA WA MAALIM SEIF WAPATA AJALI MISUNGWI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
 
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Zanzibar na Katibu Mkuu wa CUF, Seif Sharif Hamad, amenusurika  baada ya msafara wake kupata ajali iliyojeruhi viongozi wawili wa CUF.
Hata hivyo  taarifa hiyo hakutaja kuwa amejeruhiwa, kwenye ajali hiyo iliyotokea Misungwi jana.

Mkurugenzi wa Habari wa CUF, Adam Kambaya, alisema na kunukuliwa kwenye mtandao wa Mabadiliko Forum akifahamisha kuwa Katibu wa CUF Wilaya ya Nyamagana, Rehema Mwenda amepelekwa katika Hospitali ya Bugando baada ya kujeruhiwa kwenye ajali hiyo.

Kiongozi mwingine aliyejeruhiwa ni Mkuu wa Kitengo cha Habari Wilaya, aliyetajwa jina moja la Shido.

Alisema ajali hiyo ilihusisha magari mawili ya kati ya saba ya msafara wa kiongozi huyo ambayo yaligongana na lori lenye tela.

Kambaya alisema Shido pia ni Mwenyekiti wa Mtaa Utemini kata ya Mirongo, alipelekwa Bugando pia.
SOURCE: NIPASHE

0 comments:

Post a Comment

 
Support by Tone multimedia company Limited
Copyright © 2012. Zanzibar Yetu - All Rights Reserved
Designed by by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa