Home » » MSAMIATI WA UZANZIBARI WAMKERA NAIBU KATIBU MKUU UVCCM

MSAMIATI WA UZANZIBARI WAMKERA NAIBU KATIBU MKUU UVCCM

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

NAIBU Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Zanzibar Shaka Hamdu Shaka amewatahadharisha wananchi kisiwani Pemba kutowasikiliza wanaoutumia msamiati wa uzanzibari kuwagawa.
Shaka aliyasema hayo wakati akizungumza na wanachama wa Jumuiya ya UVCCM huko Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Alisema wapo waheshimiwa ambao wamekuwa wakijifanya watetezi wa uzanzibari na kusema wengi wao wakiwa ni wenye asili ya Bara.
“Mpelekeeni salamu (anamtaja jina), mwambieni aache kujifanya wakili wa kujitolea kwa kutaka kuisemea Zanzibar, asipande mbegu ya ubaguzi na mgawanyiko katika jamii,Tanganyika na Zanzibar zilikuwa moja na zitabaki hivyo milele,” Alisema Shaka huku akipigiwa makofi na wana CCM.
Aidha katika hotuba yake alisema hakuna mtu yeyote aliyezaliwa Zanzibar asiwe na sili au nasaba na Tanzania Bara, Malawi, Kongo, Burundi, Kenya au Rwanda na kwamba matamshi ya kujifanya ni Mzanzibari halisi yanahitaji kupuuzwa.
Naibu huyo aliwaambia wanachama kwamba msamiati wa uzanzibari unaweza kuwa kirusi hatari kinachoweza kuleta mgawanyiko wakati karibu nusu ya watu kutoka Pemba na Unguja hivi sasa wanaishi katika mikoa yote ya Tanzania Bara.
Akizungumzia mchakato wa Katiba, Shaka alisema anaamini Katiba mpya ya Tanzania itapatikana kutokana na uwakilishi mkubwa wa wananchi ulioko katika Bunge Maalum la Katiba linaloendelea huko Dodoma.
Shaka alisema ni jambo lisilowezekana kwa kikundi kidogo cha watu kikafanikiwa kuzuia matakwa na kukwamisha utashi wa wengi kwa sababu zisizo na msingi wala mashiko ya nguvu ya hoja.
Chanzo;Habari Leo 

0 comments:

Post a Comment

 
Support by Tone multimedia company Limited
Copyright © 2012. Zanzibar Yetu - All Rights Reserved
Designed by by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa