Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akicheza bao la kete na mzee Abdalla Salim Kitambo wa Wilaya ya Mjini wakati alipofika kuyafunga mashindano ya fainali ya mchezo huo na mchezo wa Karata katika viwaja vya Eacrotanal leo.
Baadhi ya Timu mbali mbali za Michezo ya Bao la Kete na karata wakiwa katika fainali ya michezo hiyo iliyofanyika leo katika viwanja vya Eacrotanal Mjini Unguja,wakati mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
Timu za mchezo wa karata kutoka kibanda mawazo Miembeni Chake chake Pemba na kwamtipura Unguja zikichuana katika fainali iliyofanyika leo katika viwanja vya Eacrotanal Mjini Unguja,mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza na vikundi mbali mbali vya michezo ya bao na karata wakati wa fainali ya michezo hiyo iliyochezwa leo katika viwanja vya Eacrotanal Mjini Unguja
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimkabidhi kombe bingwa wa mchezo wa Bao la Kete Kidodi Salum Kidodi wa klabu ya Mwembeladu baada ya kumfunga mpinzani wake katika fainali Mzee Nassor Othman wa klabu ya Bora imani ya Jangombe wilaya ya Mjini iliyochezwa leo katika viwanja vya Eacrotanal Mjini Unguja
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimkabidhi kombe bingwa wa mchezo wa mwakilishi wa Klabu ya Karata ya Kibanda Mawazo kutoka Miembeni Chake chake Pemba Bw,Salum Omar Ussi baada ya klabu hiyo kuwafunga klabu ya Kwamtipura katika mchezo wa fainali uliochezwa leo katika viwanja vya Eacrotanal Mjini Unguja. Picha na Ikulu.
0 comments:
Post a Comment