Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Gavana wa Benki Kuu ya Taanzania (BoT), Prof. Benno Ndulu
Hali hiyo ilijidhihirisha wazi kwa mara nyingine jana wakati wa
semina maalum iliyoandaliwa na Bunge Maalum la Katiba kwa wajumbe wa
Bunge hilo.
Semina hiyo ambayo watoa mada wakuu walikuwa, Gavana wa Benki Kuu
ya Taanzania (BoT), Prof. Benno Ndulu, na makatibu wakuu wa Wizara ya
Fedha, Dk. Servacius Likwelile upande wa wa Tanzania Bara na Khamis
Mussa, upande wa Zanzibar, iliitishwa ili kutoa ufafanuzi kwa wajumbe wa
Bunge hilo ambao wamekuwa katika sintofahamu kubwa juu ya suala hilo
wakati wa mijadala kwenye kamati zao kiasi cha kutofikia mwafaka.
Ndulu na Makatibu wakuu hao waliitwa kutoa ufafanuzi huo baada ya
kuibuka mvutano kwa wajumbe hao na kusababisha baadhi ya kamati kuacha
kiporo cha Sura ya 14 ya rasimu ya Katiba baada ya kukosa mafikiano juu
ya muundo wa benki kuu na uanzishwaji wa mfuko wa fedha wa pamoja.
Habari kutoka ndani ya semina hiyo zinasema kuliibuka mvutano mkali
juu ya mgawanyo wa fedha hizo unavyopaswa kuwa baina ya Katibu Mkuu wa
Wizara ya Fedha Zanzibar na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania pamoja na
wajumbe wa Tanzania Bara na Zanzibar
Chanzo chetu cha habari kutoka ndani ya semina hiyo, kilieleza kuwa
wakati upande wa Zanzibar ulitaka ziundwe Benki tatu ya Zanzibar,
Tanzania Bara na Muungano, wajumbe wa Tanzania bara walipinga na kueleza
kukubali muundo huo ni sawa na kurejea kwenye rasimu ya serikali tatu.
“Ndani kulikuwa na mvutano mkali, hata makatibu wa Fedha
walionekana kutofautiana kimsimamo kuhusu namna ya muundo wa benki kuu,”
kilisema chanzo hicho.
Hata hivyo, Gavana Ndulu, aliwaeleza wajumbe hao kwamba mfumo wa
kuwa na Benki kuu tatu kwa mfumo wa serikali mbili ambao umependekezwa
kwenye kamati badala ya mfumo wa serikali tatu ambao upo katika Rasimu
ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba ni kitu ambacho hakiwezekani.
“Profesa Ndulu, alituambia ubaya wa muundo uliopendekezwa na rasimu
kuwa na Benki kuu kwa kila nchi washirika, alisisitiza mfumo wa sasa
unakidhi mahitaji,” kilisema.
Akitoa maoni yake binafsi kuhusu semina hiyo, Mjumbe wa Bunge hilo,
Hamis Dambaya, alisema kutofautiana kulitokana na baadhi ya watu
kutokuwa na uelewa wa mambo ya kiuchumi na lugha za kitaalamu kuhusu
fedha.
“Wataalamu wametueleza ubaya wa muundo wa Benki kuu kuwa tatu,
walituambia kwa nini serikali ya Muungano inakopa na ile ya Zanzibar
haina fursa hiyo, wote tumeelewa tunasubiri kurudi kwenye kamati zetu
kutatua suala hili,” alisema Dambaya.
Aidha, Dambaya, alisema ufafanuzi huo uligusa katika suala la
mgawanyo wa mapato, ambapo wamegundua inakwenda vizuri tofauti na maneno
yanayotolewa nje ya Bunge hilo.
Chanzo hicho, pia kilisema Katiba Mkuu wa Wizara ya Fedha Zanzibar,
Mussa, alionekana kutofautiana na Profesa Ndulu kuhusiana na suala la
kuwa na benki tatu.
SOURCE:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment