Marubani
wawili wamefariki Dunia katika ajali ya ndege wakati wa kurusha ndege
baada ya matengezo katika Uwanja wa Ndege wa Abeid Amani karume.
Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo lililotekea jana majira ya saa saba Mchana
Uwanjani hapo, Muhandisi Mkuu kutoka kampuni ya Tropical Air, David
Kisusi amesema ndege hiyo imeanguka na kuungua na kusababisha vifo kwa
marubani hao ambao walikuwa ndani ya ndege hiyo.
Amesema
ndege hiyo yenye usajili wa 5H-TDF yenye uwezo wa kubeba abiria wanne
ni mali ya Chuo cha Usafirishaji cha Dar-es-Salam (NIT) ambayo ilikuwepo
Zanzibar kwa ajili ya matengenezo.
Daktari
Bingwa wa Uchunguzi katika Hospital ya Kuu ya Mnazi mmoja, Msafiri
Marijani amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo na amesema vifo hivyo
vimesababishwa na kukosa hewa safi wakati wa ajali hiyo pamoja na
kathirika na moto uliotokea wakati wa kuanguka ndege hiyo.
Amesema
uchunguzi ulifanywa katika miili ya maiti hao mnamo majira ya saa 12:45
jioni pia ulitokana na kukosa msaada wa kwa muda mrefu tangu ndege hiyo
ianguke na kulipuka.
Wakati
huohuo Mkuu wa Chuo cha Usafirishaji wa Anga kutoka Dar es Salaam, Dkt.
Bwire Rufunjo alifika Zanzibar kwa ajili ya kufuatilia taarifa za ajali
hiyo na amesema wamepokea taarifa hiyo kwa mshtuko mkubwa kutokana na
vifo vya wafanyakazi hao muhimu katika sekta ya anga.
Aliwataja
marehemu kuwa ni Injinia Edger Alfred Mecha mwenye Umri wa miaka 26 na
mwengine ni Dominic Bomani mwenye umri wa miaka 64 ambao walikuwa
wanafanya kazi katika chuo hicho kwa ufanisi mkubwa.
Aidha
amewataka wanafamilia wa Marehemu hao kuwa wavumilivu katika kipindi
hichi kigumu kufuatia msiba huo pamoja na kutoa wito kwa wanafunzi wa
chuo hicho kutokata tamaa wakati wa masomo.
Akizungumzia
sababu ya kuanguka kwa ndege hiyo ndogo, amesema uchunguzi bado
unaendelea lakini katika uchunguzi wa awali wamebaini kuwa ni hitilafu
ya mfumo wa umeme ambao umesababishwa na moto ulilipuka kutokana na
ndege kuwa na Mafuta mengi.
Ndege
hiyo imenunuliwa kutoka kampuni ya Tropical Air ya Zanzibar kwa ajili
ya kufundishia Urubani katika Chuo cha Usafirishaji lakini kutokana na
kutokuwa na hali Nzuri ililazimika kufanyiwa matengenezo na kampuni hiyo
kabla kuchukuliwa na chuo.
0 comments:
Post a Comment