Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Naibu waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar Mahamoud
Thabiti Kombo amesema bodi ya Chakula, Madawa na Vipodozi inajenga
maabara ya kisasa ya uchunguzi wa madawa , chakula na vipodozi ambayo
itakuwa na ubora wa Kimataifa.
Hayo ameyasema leo huko Baraza la Wawakilishi nje kidogo ya
Mji wa Zanzibar
wakati akijibu swali la Mwakilishi wa Jimbo la Muyuni Mhe. Jaku Hashimu Ayoub
aliyetaka kujua kwamba bodi ya Chakula, Madawa na Vipodozi ni taasisi muhimu
kwa afya za binaadamu, kwanini Wizara haifikirii kuipa ruzuku na lini watawapa
ruzuku hizo.
Alisema
ruzuku ya bodi
hiyo itapatiwa katika bajeti ijayo na zaidi ya
milioni 70 zimetengwa kuipa bodi hiyo ili kuyafikia mahitaji yao ikiwa
pamoja na ujenzi huo wa maabara.“Hivi sasa bodi wana tengeneza laborali
ya kisasa inayoweza
ushindani kuvipima vyakula vinavyoingia nchini”,alisema Naibu Waziri
huyo.
Aidha Naibu Waziri huyo alisema kuwa hakuna ruhusa ya
chakula, dawa na vipodozi kuingia dukani bila ya bodi hiyo kuvifanyia uchunguzi
wa kimaabara na pale vitu hivyo vinapobainika kuwa ni vibovu ndio bodi huchukua
jukumu la kuviangamiza.“Inapobainika kuwa chakula, Madawa na vipodozi ni vibovu
basi mmiliki hupigwa faini kwanza na baadae hulazimika alipie kazi ya
uangamizaji”, alisema Mahamoud.
Wakati huo Naibu Waziri huyo kwa niaba ya Waziri wa Afya alitoa
tarifa fupi ya dharura juu ya ukosekanaji wa maji katika Hospitali ya Mnazi
Mmoja ambayo ilileta usumbufu mkubwa hospitalini hapo.Hata hivyo alisema huduma hiyo tayari imeshapatiwa ufumbuzi
kwa ushirikiano na mafundi wa Mamlaka ya Maji Zanzibar ambapo huduma hiyo inapatikana bila ya usumbufu.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO- ZANZIBAR
0 comments:
Post a Comment