Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Jimbo lake lafutwa na tume, baadhi ya waliogombea majimbo ya zamani sasa yamebadilishwa majina.
Muhammed Habibu Mnyaa.
Mkurugenzi wa uchaguzi wa chama hicho, Omar Ali Shehe, alisema
baada ya Zec kufanya mabadiliko ya mgawanyo wa majimbo na kuongeza
majimbo manne mapya, chama hicho kililazimika kufanya mabadiliko ya
wagombea wa majimbo.
Alisema baadhi ya wagombea waliogombea majimbo ya zamani na sasa
yamebadilishwa majina wamewapa majimbo hayo yaliobadilishwa majina na
kuwaongeza wagombea wanne kwa majimbo mapya kwa nafasi za uwakilishi.
Mnyaa alikataliwa na wananchi katika kura za maoni, lakini baadaye
Baraza Kuu la Uongozi likapitisha jina lake kugombea nafasi hiyo, hatua
iliyoibua malalamiko kutoka kwa wanachama wa CUF kwa madai ya kuwa
hakuwa chaguo lao.
Baraza Kuu la CUF lilirejesha jina la Mnyaa kabla ya Zec kutoa
ripoti ya mapitio na mgawanyo wa majimbo na baada ya kumaliza kazi hiyo
tume ililifuta jimbo la Mkanyageni alilokuwa akiliongoza.
Shehe alisema jana kuwa utaratibu uliotumika katika kuwapata
wagombea wa majimbo mapya wamefuata katiba ya chama ambayo inaruhusu
kufanya mabadiliko katika hali ya dharura.
Aidha, CUF imemrejesha Naibu Naziri wa Ardhi, Makaazi, Maji na
Nishati, Haji Makame Mwadini ambaye alibwagwa katika kura za maoni
kutetea nafasi yake ya uwakilishi kwa jimbo la Nungwi na jina lake
halikurejeshwa na Baraza Kuu la chama hicho, lakini sasa amepewa
kugombea jimbo la Kijini.
Waliobadilishwa majimbo baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec)
kutaja majina mapya kwa baadhi ya majimbo ni Mji Mkongwe, Ismail Jussa
Ladhu (sasa Malindi) wakati ni Ali Saleh aliyekuwa anagombea ubunge Mji
Mkongwe (sasa Malindi).
Wengine ni mwakilishi wa jimbo la Mtoni, Nassor Ahmed Mazrui
amepelekwa jimbo la Mtopepo, Mansour Yussuf Himid uwakilishi jimbo la
Chukwani badala ya Kiembe Samaki na Abdillahi Jihadi Hassan uwakilishi
jimbo la Mwanakwerekwe badala ya Magogoni
CHANZO:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment