Sheikh Thabit Nooman Jongo kutoka
Afisi ya Mufti Zanzibar akiwafahamisha jambo washiriki wa mafunzo ya
Haki za Binaadamu katika Ukumbi wa Mazsons Hotel mjini Zanzibar.
Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh
Saleh Omar Kaabi wakwanza kushoto akitoa maelezo juuya haki za
binaadamu kwa mujibu wa Uislam wakati alipokuwa akifunguwa Mafunzo ya
Haki za Binaadamu na kuwatambulisha wasaidizi wa Sheria kwa Viongozi wa
Dini, katikati ni Mkurugenzi Mtendaji Harusi Miraji na mwisho Jina
Mwinyi Waziri Afisa Mipango wa Kituo cha Huduma na Sheria.
………………………………………………..
Na Miza Othman –Maelezo Zanzibar
Mashekhe na Walimu wa Madrasa
wametakiwa kuwashajihisha Wananchi ili waepuke kujiingiza katika makundi
yanayoweza kuvunja amani katika kipindi hiki cha Mchakato wa Uchaguzi
Mkuu nchini.
Hayo yameelezwa na Mufti Mkuu wa
Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kaabi alipokuwa akifunguwa mafunzo ya Haki za
Binaadamu yaliyoandaliwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar na
kufanyika katika ukumbi wa Mazsons Hotel,Shangani Mjini Zanzibar.
Amesema Masheikh na Walimu hao
ndio Wasimamizi wakuu katika maeneo mbalimbali ikiwemo Miskitini,
Madrasani na hata ndani ya Nyumba zao kwani kufanya hivyo kutawasaidia
kuepuka Uvunjifu wa Amani ni.
“Tofauti za dini, jinsia, cheo na
Kabila sio njia za ukiukwaji wa Sheria ndani ya Nchi yetu bali zitumike
katika kutii sharia kwa kila raia”,alisema Shekh Kaabi.
Nae Shekh Thabit Nooman Jongo
kutoka Afisi ya Mufti Zanzibar amewataka Walimu na Mashekhe wenzake kuwa
mstari wa mbele katika kusimamia juu ya ukumbusho huo kwani kufanya
hivyo ni kutekelaza majukumu yao.
Aidha amewataka Masheikhe na
Walimu hao kuchukuwa juhudi za hali ya juu na kutumia maneno ya hekima,
busara na unyenyekevu ili waweze kufanikiwa malengo waliyokusudia.
Hata hivyo amesema kuwa wakati
wanapotoa hutuba zao ndani ya Misikiti na Madrasa ziwe ni zenye kujenga
amani kwani kufanya hivyo ni kuzitii sheria zilizowekwa katika nchi yao.
Kwa upande wao Washiriki wa
mafunzo hayo wamesema watayafanyia kazi bila ya kinyongo na kuyafikisha
katika maeneo yao kama walivyoagizwa na Viongozi wenzao.
0 comments:
Post a Comment