Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima akitoa hotuba fupi
ya kuwakaribisha nchini wajumbe wa Baraza la Mawaziri wa Nchi za Maziwa
Makuu na Pembe ya Afrika katika Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti
Uzagaaji wa Silaha Haramu (RECSA) kabla ya kufungua kikao cha wajumbe
hao kinachofanyika katika Hoteli ya Sea Cliff, Zanzibar. Lengo la kikao
hicho ni kujadili masuala mbalimbali ya jinsi ya Mapambano ya Kuzuia na
Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu katika nchi wanachama ambazo ni
Burundi, Congo, Djibout, Ethiopia, Eritrea, Kenya, Rwanda, Sudan,
Uganda, Sudan, Sudan Kusini, Seychelles, Afrika ya Kati, Somalia na
Tanzania. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Wajumbe
wa Baraza la Mawaziri wa Nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika katika
Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu (RECSA)
wakiwa katika chumba cha mkutano wakijadili masuala mbalimbali ya jinsi
ya Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu katika
nchi wanachama ambazo ni Burundi, Congo, Djibout, Ethiopia, Eritrea,
Kenya, Rwanda, Sudan, Uganda, Sudan, Sudan ya Kusini, Seychelles, Afrika
ya Kati, Somalia na Tanzania.
Mkutano
huo unafanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Sea Cliff,
Zanzibar ambapo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe
(hayupo pichani) ndio Mwenyekiti wa Baraza hilo, hata hivyo katika
Mkutano huo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima
(kulia meza kuu) anamuwakilisha katika kikao hicho.
Mwakilishi
wa Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya
Afrika katika Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha
Haramu (RECSA) na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchini, Pereira Ame
Silima (kulia) akiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Uganda ambaye
pia ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo, Balozi James Baba (katikati) na
Mjumbe wa Baraza hilo ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Usalama wa
Ndani nchini Rwanda, Balozi Munyabagisha Valeus, wakisoma taarifa za
masuala mbalimbali ya jinsi ya Kupambana ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji
wa Silaha Haramu katika nchi wanachama ambazo ni Burundi, Congo,
Djibout, Ethiopia, Eritrea, Kenya, Rwanda, Sudan, Uganda, Sudan, Sudan
Kusini, Seychelles, Afrika ya Kati, Somalia na Tanzania. Baraza hilo
limekutana katika Hoteli ya Sea Cliff, Zanzibar leo.
Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Nchi za Maziwa
Makuu na Pembe ya Afrika katika Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti
Uzagaaji wa Silaha Haramu (RECSA) na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani wa
Nchi nchini, Pereira Ame Silima (katikati waliokaa) akiwa katika picha
ya pamoja na Wajumbe wa Baraza hilo ambalo nchi zake wanachama ni Congo,
Djibout, Ethiopia, Eritrea, Kenya, Rwanda, Sudan, Uganda, Sudan, Sudan
Kusini, Seychelles, Afrika ya Kati, Somalia na Tanzania. Wajumbe hao
wamekutana katika Hoteli ya Sea Cliff, Zanzibar leo. Picha zote na Felix
Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.
0 comments:
Post a Comment