Mkufunzi
na Mwandishi Mkongwe wa Tasnia ya Habari Zanzibar Salim Said Salim
akitoa mada katika mafunzo ya siku tano juu ya kuandika Habari za
Uchaguzi Mkuu yaliyoandaliwa na Shirika la Habari la Marekani
Internews kwa waandishi wa Habari wa Zanzibar katika Ukumbi wa Umoja
wa watu wenye Ulemavu Kikwajuni Mjini Zanzibar. Picha na Makame
Mshenga-Maelezo Zanzibar.
Mhadhiri
wa Sheria, Kitivo cha Sheria Zanzibar University, Ali Uki akionyesha
kitabu cha Sheria cha Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) na kitabu cha
Sheria cha Tanzania na cha Zanzibar ambavyo vinawapasa waandishi wa
habari kuvisoma na kuzitumia sheria hizo katika kuandika habari za
Uchaguzi Mkuu kwa usahihi.
Mhadhiri
wa Sheria, Kitivo cha Sheria Zanzibar University, Ali Uki akisisitiza
kitu kwa waandishi wa Habari katika mafunzo yaliyoandaliwa na Shirika la
Internews katika Ukumbi wa Umoja wa watu wenye ulemavu Kikwajuni Mjini
Zanzibar.
Baadhi
ya waandishi wa habari walioshiriki mafunzo juu ya kuripoti Habari za
Uchaguzi kutoka vyombo mbali mbali vya Serikali na binafasi wakifuatilia
mada zilizokuwa zikiwakilishwa.
Afisa
Mwandamizi Baraza la Habari Tanzania Ofisi ya Zanzibar Shifaa Said
Hassan akiwasilisha mada ya wajibu wa vyombo vya habari katika kuripoti
Uchaguzi Mkuu katika mafunzo ya waandishi wa Habari yanayofanyika Ukumbi
wa Umoja wa watu wenye ulemavu Kikwajuni Mjini Zanzibar.
Mtayarisha
na Mtangazaji wa vipindi wa Redio Zenj FM Mustapha Mussa akitoa mchango
katika mafunzo hayo yanayofanyika Ukumbi wa watu wenye ulemavu
Kikwajuni Zanzibar.
Washiriki wa mafunzo ya kuripoti Uchaguzi Mkuu wakiwa katika kazi za vikundi wakijadiliana katika kufanikisha mafunzo hayo.
Mwandishi
wa Habari wa Gazeti la Zanzibar Leo Hafsa Golo akiwasilisha mada ya
grop lake katika mafunzo ya kuandika Habari za Uchaguzi Mkuu
yaliyoandaliwa na Shirika la Habari la Ineternews la Marekani katika
Ukumbi wa Umoja wa watu wenye ulemavu Kikwajuni Mjini Zanzibar.
Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
0 comments:
Post a Comment