Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Msajili
wa vyama vya siasa Tanzania Jaji Francis Mutungi, akizungumza na Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, nyumbani
kwake Mbweni Zanzibar.
Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwa
katika picha ya pamoja na Msajili wa vyama vya siasa Tanzania Jaji
Francis Mutungi (wa pili kushoto) na baadhi ya wajumbe wa Ofisi hiyo.
Kushoto ni msajili wa vyama Zanzibar Bw. Rajab Baraka. (Picha na Salmin
Said, OMKR)
Na: Hassan Hamad, OMKR.
Msajili
wa vyama vya siasa Tanzania Jaji Francis Mutungi, amesema kuna umuhimu
kwa viongozi wa vyama vya siasa Zanzibar kukutana, ili kutatua mzozo wa
kisiasa uliojitokeza.
Amesema
Zanzibar ni nchi amani, hivyo hakuna haja ya kuruhusu migogoro ya aina
hiyo ambayo inaweza kupelekea kuvurugika kwa amani na kuipotezea sifa
Zanzibar katika jamii ya Kimataifa.
Jaji
Mutungi akiambatana na baadhi ya wajumbe wa ofisi hiyo ya msajili
pamoja na msajili wa vyama kwa upande wa Zanzibar Bw. Rajab Baraka,
ametoa ushauri huo wakati akizungumza na Makamu wa Kwanza wa Rais wa
Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, nyumbani kwake Mbweni, nje
kidogo ya mji wa Zanzibar.
Amesema
kuna kila sababu ya kulinusuru taifa kuingia katika migogoro isiyokuwa
ya lazima, na kutaka juhudi za makusudi zichukuliwe ili kumaliza tatizo
hilo.
Kwa
upande wake Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif
Sharif Hamad ambaye pia ni mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CUF,
amesema amekuwa akichukua juhudi binafsi kukutana na wagombea wenzake
kuzungumzia tatizo hilo, lakini baadhi yao wanaonekana kutokuwa tayari
kulizungumza.
Amesema
hapendi kuona Zanzibar inaingia katika machafuko yanayoweza kuepukwa,
na kwamba viongozi wengine pia wanapaswa kufikiria amani na maslahi ya
Zanzibar kuliko maslahi binafsi.
Katika
hatua nyengine Maalim Seif amemshutumu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi
ya Zanzibar (ZEC) Bw. Jecha Salim Jecha kwa kuiingiza nchi katika
migogoro ya kisiasa na kikatiba.
Akinukuu
vipengele vya Katiba ya Zanzibar, Maalim Seif amesema kipindi cha Urais
wa Zanzibar ni miaka mitano kuanzia tarehe ya kuapishwa, hivyo kuanzia
tarehe 02/11/2015 kipindi cha Urais wa Zanzibar awamu ya saba kitakuwa
kimemalizika.
Hivyo
amesema bila ya kuchukuliwa juhudi za dharura, kuanzia tarehe 02 mwezi
ujao kwa mujibu wa katiba, Zanzibar itakuwa haina Rais, Serikali wala
Baraza la Wawakilishi.
0 comments:
Post a Comment