Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Awa
Dabo (kulia) na Mkuu wa ofisi ndogo ya Umoja wa Mataifa Zanzibar, Anna
Senga (katikati) wakimkaribisha mmoja wa wageni waalikwa katika sherehe
za kutimiza miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa iliyofanyika
katika Hoteli ya Serena Shangani Mjini Zanzibar mwishoni mwa wiki.(Picha
na Zainul Mzige wa Modewjiblog).
Na Mwandishi wetu, Zanzibar
SERIKALI
ya mapinduzi Zanzibar imesema kuwa itaendelea kuthamini fursa mbali
mbali zinazotolewa na Umoja wa Mataifa (UN) ili ziweze kuwanufaisha
wananchi wote bila ya ubaguzi.
Kauli
hiyo imetolewa na Waziri wa nchi Ofisi ya Rais, Kazi na Utumishi wa
Umma, Haroun Ali Suleiman wakati akihutubia katika sherehe za kutimiza
miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa iliyofanyika katika
Hoteli ya Serena Shangani Mjini Zanzibar, alisema umoja huo umekuwa
sekta muhimu ya kuunga mkono juhudi za maendeleo ya serikali katika
sekta mbali mbali za kiuchumi, kijamii na kisiasa.
Alisema
kuwa Zanzibar ikiwa miongozi mwa nchi zinazoendelea barani Afrika
inaendelea kutumia vizuri fursa zinazotolewa na umoja huo kwa lengo la
kujenga jamii bora zenye kipato na uwezo wa kati kwa lengo la kupunguza
umasikini nchini.
Waziri
Haroun alifahamisha kuwa miradi mbali mbali ya maendeleo inayotolewa na
umoja huo imekuwa nyenzo muhimu ya kuisaidia serikali kuhudumia
wananchi wake kwa ufanisi zaidi.
Alisema
kutokana na misaada hiyo Zanzibar pia imekuwa mdau muhimu wa umoja huo
kwani ni miongoni mwa nchi yenye urithi wa kimataifa kupitia maeneo ya
Mji Mkongwe jambo ambalo ni ishara tosha ya mahusiano mema kati ya umoja
huo na serikali.
Wafanyakazi
wa Umoja wa Mataifa visiwani Zanzibar wakibadilishana mawazo wakati wa
kuwasili kwa wageni waalikwa kwenye sherehe hizo.
“
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inajali kwa kiasi kikubwa juhudi za
Umoja wa Mataifa kwa kutuunga mkono, nasi tunaendelea kutumia vizuri
miradi mnayotuunga mkono.
Pia
tunaendelea kukuombeni mtusaidie pale tutakapohitaji msaada wenu kwa
Nyanja tofauti kwani bajeti ya serikali haitoshi kukidhi mahitaji yote
ya kuendesha serikali.”, Alisema Waziri Haroun.
Naye
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez alikiri kuridhishwa kwake
na utekelezaji wa miradi mbali mbali ya umoja huo na kuahidi kuendelea
kushirikiana vizuri na serikali ili kufikia dhana ya maendeleo endelevu
Tanzania na Zanzibar kwa ujumla.
Bw.
Rodriguez alibainisha kuwa umoja huo bado unaendelea kufanya tathimini
na utafti juu ya masuala mbali ya kisiasa na kijamii nchini ili kuona ni
kwa jinsi gani watasaidia kuunga mkono maeneo hayo kwa maendeleo ya
nchi.
Alifafanua
kuwa katika miradi mbali mbali iliyotekelezwa Zanzibar kupitia
mashirika ya Umoja huo hasa UNDP, UN WOMEN na UNESCO miradi hiyo imeweza
kufanikiwa zaidi ya asilimia 80 jambo ambalo ni faraja kwa umoja huo.
Kila mtu alikuwa na tabasamu la furaha....Happy Birthday #UN70
Alieleza
kuwa kupitia dhana ya maendeleo endelevu kwa mwaka 2016 umoja huo
umejipanga kusaidia masuala mbali mbali ya haki za binadamu, utawala
bora, uwazi na uwajibikaji, afya na vipaumbele vya kisera kwa serikali
ili kuhakikisha Zanzibar inakuwa ni nchi ya kupigiwa mfano kimaendeleo.
“
Tuna kila sababu za kuishukru serikali ushiriki wake katika miradi yetu
kwani bila wao kutuunga mkono vizuri leo hii tusingweza kuwepo hapa
kusherekea mafanikio tuliyopata ndani ya miaka 70 ya UN hivyo nasi
tunaahidi kuenzi mahusiano haya kwa lengo la kujenga jamii bora.”,
alisema Bw.Rodriguez.
Aidha
aliishauri serikali kuhakikisha mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu
unafanyika kwa amani na kwa kuzingatia vigezo vya uwazi, uhuru na haki
ili kila chama kilichoshiriki katika mchakato huo kinapata haki yake kwa
mujibu wa sheria za nchi.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kulia) akiteta jambo na Mkuu
wa ofisi ndogo ya Umoja wa Mataifa Zanzibar, Anna Senga.
“
Tunawatakieni uchaguzi mwema na wenye mafanikio bila ya kuwepo dalili
za uvunjaji wa haki za binadamu ama kiashiria chochote cha vurugu ili
muendelee kulinda heshima na mafanikio yaliyopatikana katika Serikali ya
Umoja wa Kitaifa (SUK).” alisisitiza Bw. Rodriguez.
Sherehe
hizo za kutimiza miaka 70 za UN zilifanyika katika ukumbi wa hoteli ya
Serena Mjini Zanzibar na kuwashirikisha wadau mbali mbali wa umoja huo
wakiwemo wawakilishi wa mashirika ya kimataifa yanayofanya kazi Zanzibar
na kutoa Tuzo na vyeti vya kumbu kumbu kwa taasisi na shule
zilizoshiriki kikamilifu katika utekelezaji wa baadhi ya miradi ya umoja
huo.
Ofisa
anayeshughulikia masuala ya ushirikiano wa WHO Zanzibar, Dkt. Ghirmay
Andemichael (kushoto) akibadilishana kadi na mmoja wa wageni waalikwa
(ambaye jina lake halikuweza kupatikana kirahisi).
Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Awa
Dabo (kushoto) akifurahi jambo na Mgeni rasmi Waziri wa nchi Ofisi ya
Rais, Kazi na Utumishi wa Umma, Haroun Ali Suleiman.
Mgeni
rasmi Waziri wa nchi Ofisi ya Rais, Kazi na Utumishi wa Umma, Haroun
Ali Suleiman (kulia) na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa
na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez
wakizindua rasmi malengo ya Maendeleo Endelevu 17 ( SDGs) katika sherehe
za kutimiza miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa iliyofanyika
katika Hoteli ya Serena Shangani Mjini Zanzibar mwishoni mwa wiki.
Fataki zikipamba uzinduzi huo, sasa yamezinduliwa rasmi.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez akitoa salamu za Umoja wa
Mataifa katika sherehe za kutimiza miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Umoja
huo.
Baadhi
ya wakuu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa Dar na Zanzibar wakimsikiliza
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo (UNDP) nchini, Bw.Alvaro Rodriguez (hayupo pichani) wakati
akitoa salamu za UN katika sherehe za kutimiza miaka 70 tangu
kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa iliyofanyika katika Hoteli ya Serena
Shangani Mjini Zanzibar.
Mgeni
rasmi Waziri wa nchi Ofisi ya Rais, Kazi na Utumishi wa Umma, Haroun
Ali Suleiman akitoa salamu za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika
sherehe za kutimiza miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa
iliyofanyika katika Hoteli ya Serena Shangani Mjini Zanzibar.
Mgeni
rasmi Waziri wa nchi Ofisi ya Rais, Kazi na Utumishi wa Umma, Haroun
Ali Suleiman na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na
Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Bw.Alvaro Rodriguez
pamoja na wakuu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini wakifanya
'Toast' katika kilele cha sherehe za kutimiza miaka 70 tangu kuanzishwa
kwa Umoja wa Mataifa iliyofanyika katika Hoteli ya Serena Shangani Mjini
Zanzibar.
'Toast' hiyo iliambatana na milipuko ya Fataki kusherehesha miaka 70 ya Umoja wa Mataifa tangu kuanzishwa kwake. Kwa picha zaidi bofya link hii
0 comments:
Post a Comment