Home » » WALIMU WA SKULI MBALI MBALI ZA WILAYA WAPATIWA MAFUNZO YA MICHEZO NA KAMATI YA OLIMPIKI TANZANIA (TOC) MJINI ZANZIBAR

WALIMU WA SKULI MBALI MBALI ZA WILAYA WAPATIWA MAFUNZO YA MICHEZO NA KAMATI YA OLIMPIKI TANZANIA (TOC) MJINI ZANZIBAR

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Mkufunzi wa Mafunzo ya Walimu wa Michezo wa Skuli yaliyoandaliwa na Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) Suleiman Mahmoudu Jabiri akitowa maelezo kwa washiriki katika siku ya mwisho ya mafunzo hayo yaliyoanza tarehe 01 mwenzi huu.Mkurugenzi wa Idara ya Elimu mbadala na Watu wazima Mashavu Fak akifunga mafunzo ya walimu wa michezo wa Skuli katika Skuli ya Elimu Mbadala Rahaaleo Mjini Zanzibar.Mkurugenzi wa Idara ya Elimu mbadala na Watu wazima Mashavu Faki akiwakabidhi vyeti washiriki wa mafunzo yaliyoandaliwa na Kamati ya TOC katika Ukumbi wa Elimu Mbadala Rahaleo Mjini Zanzibar.


Na Rahma Khamis Maelezo Zanzibar

Idara ya ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar imeshauriwa kuwaandalia michezo nje ya nchi walimu wa michezo wa skuli kwa lengo la kujipatia taaluma zaidi na kukukuza mechezo nchini ,

Hayo yameelezwa huko Rahaleo katika Ukumbi wa Elimu Mbadala na Watu wazima na Mkurugenzi Idaraya hiyo Zanzibar Mashavu Faki wakati akifunga mafunzo yalioandaliwa na Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) yaliyofunguliwa tarehe 1 mwezi huu.Amesema iwapo walimu wa michezo watapatiwa mafunzo zaidi nje ya nchi wataweza kuwasomesha wanafunzi wao wa skuli na kuinua sekta ya michezo Zanzibar.

Mkurugenzi Mashavu amesema katika mwaka 2013 kulifanywa utafiti wa kimchezo na kuonekana kuwa nchi zinazoimarisha michezo maskulini ndizo zinazofanya vizuri zaidi katika masomo yao.Aidha amesema michezo huimarisha afya, kujenga upendo, udugu na uzalendo katika jamii hivyo hakuna budi kuendelezwa kwa manufaa ya wanamichezo wenyewe na Taifa kwa jumla.

Sambmba na hayo Mkurugenzi huyo amewashauri waalimu waliopata mafunzo hayo kwa kushirikiana na Idara husika kuandaa mafunzo kila baada ya miezi mitatu.Nae mkufunzi wa mafunzo hayo Suleiman Mahamoud Jabir amewataka washiriki wa mafunzo hayo kujenga moyo wa kujitolea kwani katika kufundisha mara nyingi hujitokeza matatizo mengi.

Kwa upande wao waalimu waliopata mafuzo hayo Mussa Abdulrab na Arafa Talib Omar wamesema wamejifunza mambo mengi wasioyajua na kuahidi kuwa watayafanyia kazi.Mafunzo hayo ya siku tano ya walimu wa michezo wa skuli mbali mbali za Zanzibar yameandaliwa na Kamati Tanzania.

0 comments:

Post a Comment

 
Support by Tone multimedia company Limited
Copyright © 2012. Zanzibar Yetu - All Rights Reserved
Designed by by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa