Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mwanasiasa mkongwe Zanzibar, Ali Ameir Mohamed,
amesema Zanzibar ni nchi huru inayojitegenea ndani ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, hivyo haipaswi kuingiliwa wala kuhojiwa katika
mambo yake ya ndani, ikiwamo suala la kurudiwa uchaguzi mkuu wa Zanzibar
utakaofanyika Machi 20, mwaka huu.
Akizungumza na Nipashe mjini hapa jana, Ali Ameir alisema Zanzibar
ina madaraka yake, katiba yake, Rais wake, Baraza la Wawakikishi na
mahakama, hivyo haipaswi kuingiliwa katika mambo yake licha ya kuwa
shemu ya Tanzania.
Alitoa kauli hiyo baada ya kutolewa kwa tamko la nchi saba za
Jumuiya ya Ulaya zikiongozwa Marekani, kuwa hawajaridhishwa na kurudiwa
kwa uchaguzi mkuu wa Zanzibar.
Alisema mabalozi wanaowakilisha mataifa yao nchini lazima wafahamu
na kutambua kuwa Zanzibar ni nchi huru na ilipata uhuru wake uliootokana
na Mapinduzi yaliouangusha ufalme wa kigeni uliokalia visiwa hivyo kwa
miaka 160.
Alisema kitendo cha mabalozi wa nchi nyingine kuhoji uamuzi wa Tume
ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kutangaza kurudia uchaguzi ni kuingilia
mambo ya ndani ya Zanzibar, kwenda kinyume cha taratibu za kidiplomasia
na ukiukaji wa mikataba ya kimataifa.
Alisema katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 imeipa mamlaka ZEC
kuratibu, kuitisha, kusimamia na kutangaza matokeo ya uchaguzi na kwamba
maamuzi yake hayawezi kuhojiwa au kuingiliwa na mtu au mamlaka yoyote
iwe ya ndani au nje ya nchi.
Alisema uamuzi uliofanywa za ZEC kuitisha uchaguzi wa marudio
unapaswa kuheshimiwa kwa sababu yanatokana na utashi wa katiba na sheria
na kwamba hiyo ndiyo njia pekee ya kukwamua utata wa mkwamo wa uchaguz
mkuu uliofanyika Oktoba 25, mwaka jana.
CHANZO:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment