Na Mwandishi Wetu, Zanzibar.
CHAMA
cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimewasisitiza watendaji wa Chama na
Jumuiya zake kuharakisha zoezi la kuhorodhesha Mali za taasisi hizo ili
kutekeleza kwa vitendo agizo la chama hicho.
Akizungumza
na watendaji wa chama, jumuiya na watumishi wa chama hicho wa ngazi
mbali mbali , Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai huko
afisi kuu ya CCM Kisiwanduzi Unguja.
Alifafanua
kwamba hatua hiyo inatokana na agizo la Mwenyekiti mpya wa CCM Dkt.
John Pombe Magufuli aliyetaka mali za chama hicho kuhorodheshwa haraka
kwa lengo la kuimarisha chama hicho.
Alisema
kwamba CCM Zanzibar ilianza utaratibu wa kukagua mali zake kabla ya
Mwenyekiti huyo kutoa agizo hivyo anatarajia kwamba watendaji hao
watatekeleza kazi hiyo haraka na kwa mujibu wa utaratibu uliowekwa ili
kuepuka usumbufu usiokuwa wa lazima.
Alieleza
kwamba licha ya Chama kupata ruzuku kutoka serikali bado kina wajibu wa
kutumia rasilimali zake vizuri kuongeza vyanzo vya mapato ili kuongeza
ufanisi wa kiutendaji ndani ya chama hicho.
Alisema
hatua ya kuhorodhesha mali za chama hicho iambatane na kumaliza kasoro
na mapungufu yaliyopo katika miradi ya chama na jumuiya hasa kupitia
upya mikataba ya ukodishwa ili kuhakikisha inakidhi na kufuata utaratibu
wa kisheria.
“
Nawakumbusha watendaji wenzangu wa CCM kwamba tujiandae vizuri kifikra
kwa kuhakikisha tunafanya kazi kwa bidii kubwa na kuacha tabia za
kufanya kazi kwa mazoea kwani huu ni wakati wa mabadiliko kwa kila sekta
ndani ya chama chetu.
Pia
mnajua kwamba chama chetu hivi karibuni kumefanyika Mkutano Mkuu Maalum
na kumpata Mwenyekiti Mpya Dkt. Jonh Pombe Magufuli atakayesaidiana na
Makamo Mwenyekiti wake Dkt. Shein kuhakikisha wanaendeleza kuimarisha na
kukuza ustawi wa CCM, hivyo nasi ni lazima twende sambamba na kasi ya
utendaji wao.”., alisema Vuai.
Vuai
aliwataka watendaji hao kuzidisha ari na juhudi za kiutendaji kwa lengo
la kwenda sambamba na kasi ya matakwa ya utekelezaji wa Ilani ya
Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2020.
Akizungumzia
maagizo mbali mbali yaliyotolewa na CCM katika vikao mbali mbali vya
Mkutano Mkuu huo, alisema kila mtendaji ama kiongozi wa chama hicho
Zanzibar aliyeguswa na maelekezo hayo anatakiwa kuyafanyia kazi bila ya
kusubiri kuwajibishwa.
Alisema
miongoni mwa vipaumbele vya Mwenyekiti wa Chama hicho, Dkt. Magufuli ni
kuimarisha maslahi ya watumishi wa CCM ili yaeeze kwenda sambamba na
wakati uliopo kiuchumi.
Alisema
Dkt. Magufuli alikiri kuwepo kwa mazingira magumu ya kiundaji ndani ya
CCM na kuahidi kutatua changamoto hizo ili kuhakikisha wafuasi wa chama
na wananchi kwa ujumla wananufaika na sera bora zilizowekwa na chama
hicho.
Aliwasihi
watendaji hao kuongeza ushirikiano na umoja katika utekelezaji wa
majukumu yao na kuepuka majungu na fitna miongozi mwao na pakijitokeza
kasoro za kiutendaji waziwasilishe katika vikao vinavyotambulika
kikatiba ili ziweze kufanyiwa kazi.
Aidha
Naibu Katibu Mkuu huyo aliwapongeza wanachama, viongozi na watendaji wa
chama hicho kwa kuendelea kuiunga mkono CCM kwa kila hatua licha ya
kukabiliwa na changamoto za kisiasa.
Pamoja
na hayo alisema ushindi wa CCM wa mwaka 2020 unatakiwa kuanza
kuandaliwa hivi sasa kwa kuendeleza mazingira rafiki na yanayovutia ya
kiutendaji, uwajibikaji na uwazi katika shughuli mbali mbali za chama.
0 comments:
Post a Comment