Na Is-haka Omar, Zanzibar.
KAMATI
ya Siasa ya CCM Mkoa wa Magharibi kichama imeagizwa kukagua na
kusimamia vizuri utekelezaji wa ilani ya Chama ya Mwaka 2015/2020
inayotekelezwa katika majimbo ndani ya Mkoa huo ili kujiridhisha kama
zimetekelezwa kweli au la.
Agizo
hilo limetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, wakati
akizungumza na viongozi wa Kamati hiyo huko Ofisi ya Mkoa huo
iliyopo Mwera Unguja.
Alisema
kuna baadhi ya viongozi wa Majimbo hasa Wabunge, Wawakilishi na
Madiwani wamekuwa wakitekeleza Ilani hiyo vizuri na wengine kushindwa
kufanya hivyo hali inayosababisha kuongezeka kwa changamoto zisizokuwa
za lazima kwa baadhi ya wananchi.
Vuai
aliwambia viongozi wa Kamati hiyo kuwa pamoja na kufanya kazi za Chama
bado wana jukumu la kuwasimamia Wabunge na Wawakilishi kwa lengo la
kuhakikisha wanatekeleza kwa vitendo ahadi walizotoa kwa wananchi
majimboni.
“Msisubiri
kusikia katika vyombo vya habari au kuambiwa katika vikao kuwa Mbunge
ama Mwakilishi Fulani kachimbisha kisima au kajenga skuli (Shule)
badala yake nendeni wenyewe mkakague kwa kina miradi hiyo ili kupata
takwimu sahihi za utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa kila jimbo.”, alisema
Vuai.
Alisema
lengo la CCM ni kuwa na viongozi imara wanaosimamia maslahi, miongozo
na maelekezo ya chama na wenye uwezo wa kuwatumikia wananchi kwa vitendo
ndani ya Majimbo na Wadi.
Naibu
Katibu Mkuu huyo alieleza kwamba utekelezaji mzuri wa Ilani ya CCM ya
mwaka 2015/2020 ndiyo tiketi halali ya kuirejesha CCM madarakani katika
Uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka 2020.
Aliwasihi
viongozi kushirikiana na pendana na patakapotokea mtu amekosea watumie
vikao halali vya kikatiba kusululisha kasoro hizo.
0 comments:
Post a Comment