Na Is-haka Omar, Zanzibar.
CHAMA
Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimewasihi viongozi wa ngazi mbali mbali
katika Wilaya ya Kaskazini “B” kufanya vikao halali vya mara kwa mara
ili kuibua na kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu changamoto zinazowakabili
wanachama na wananchi kwa ujumla.
Nasaha
hizo zimetolewa na Katibu wa Kamati Maalum wa NEC, Idara ya Itikadi na
uenezi CCM Zanzibar Waride Bakar Jabu wakati akizungumza na wafuasi wa
Chama hicho katika Matawi ya CCM Boma Kiwengwa na Kinduni Mahonda
katika mwendelezo wa ziara ya kuimarisha chama ndani ya Wilaya hiyo.
Alisema
vikao halali vya kikatiba ndani ya Chama hicho ndio jukwaa rasmi la
kujadiliana, kushauriana na kufanya maamuzi sahihi ya kulinda na
kuimarisha uhai wa CCM .
Waride
alifafanua kwamba kutokuwepo na vikao kwa baadhi ya ngazi za
kiutendaji kunakwamisha utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 20-15/2020
kwa baadhi ya maeneo nchini.
“Sio
vizuri mambo yanayohusu Chama chetu yakajadiliwa nje ya vikao halali
wakati sehemu rasmi za kufanya hivyo zipo na kama kuna jambo la msingi
hakuna anayezuiwa kujenga hoja kupitia vikao, na tukifanya kinyume na
hivyo tutatengeneza fitna na migogoro isiyokuwa ya lazima.
Pia
kupitia vikao mtaweza kuwa na hoja ya pamoja ya kujibu baadhi ya njama
na Propaganda zinazofanywa na wapinzani katika maeneo yenu”,.
Alisisitiza Waride na kuongeza kwamba CCM itaendelea kuwa kinara wa
siasa za maendeleo na haki endapo kila kiongozi atatekeleza wajibu wake
kulingana na majukumu aliyopewa kikatiba.
Alifafanua
kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushirikiana na Chama
wametekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo nchini lakini imekuwa
haijulikani kwa baadhi ya wananchi na viongozi kutokana na kutokuwepo na
kutokuwepo na mfumo mzuri wa kupeana taarifa kupitia vikao.
Alisema chama hicho kitahakikisha
ahadi mbali mbali zilizoahidiwa katika Uchaguzi Mkuu uliopita
zinatekelezwa kabla ya mwaka 2020, ili kila mwananchi aweze kunufaika na
fursa zinazotokana na matunda ya Chama hicho.
Katibu
huyo aliahidi kuchukua hatua za makusudi kwa kuishawishi serika
kuendelea kutafuta wawekezaji wenye nia ya kuwekeza katika sekta za
Kilimo, Uvuvi na Utalii ili wananchi hasa wanaoishi vijijini waweze
kupata ajira na kuongeza kipato chao.
Kupitia
vikao hivyo, Waride aliwakumbusha wananchi umuhimu wa kulinda amani na
utulivu wa nchi pamoja na kushirikiana na viongozi wao wa majimbo na
serikali katika harakati kukuza uchumi wa Zanzibar.
Akijibu
baadhi ya hoja za wanachama wa Chama hicho, Katibu wa Kamati Maalum,
Idara ya Organazesheni ya CCM Zanzibar, Haji Mkema aliwataka Wazazi na
Walezi wa CCM ndani ya Wilaya hiyo kuwarithisha Vijana historia na
Itikadi halisi za CCM ili wawe waumini wa kweli wa Chama hicho.
Alisisitiza
umuhimu wa wanachama wa chama hicho kutumia fursa zilizowazunguka ndani
ya Wilaya hiyo zikiwemo Utalii na kilimo kupunguza changamoto ya
ukosefu wa ajira huku wakisubiri juhudi zinazofanywa na serikali
kumaliza tatizo hilo.
Aliwambia
na kuwataka vijana wa Chama hicho kuendelea kufanya kazi kwa bidii na
kuwa mfano mwema wa kuigwa katika jamii kwani wao ndio warithi wa
viongozi wanaostaafu utumishi ndani ya chama hicho.
Wakizungumza
wanachama hao, walikiomba chama kuwachukulia hatua za kinidhamu
baadhi ya viongozi wanaofanya kazi za CCM chini ya kiwango ili kuongeza
kasi ya utendaji ndani ya Wilaya hiyo.

0 comments:
Post a Comment