Na Is-haka Omar, Zanzibar.
CHAMA
Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimewataka Viongozi na Watendaji wa
Jumuiya ya Umoja wa Wanawake CCM (UWT) Tanzania kuongeza juhudi katika
kuimarisha Chama ili kiweze kushinda na kuendelea kuongoza dola katika
Uchaguzi Mkuu ujao.
Rai
hiyo imetolewa na Katibu wa Idara ya Organazesheni Afisi Kuu Zanzibar,
Nd. Haji Mkema wakati akizungumza na Watendaji wa Jumuiya hiyo kwa ngazi
za Mikoa na Wilaya za Unguja Kichama katika ziara ya kuimarisha uhai wa
Chama katika jumuiya hiyo.
Alisema
jumuiya hiyo inatakiwa kuandaa mapema mipango endelevu ya kuimarisha
chama kwa kuongeza wanachama wapya ndani ya chama na Jumuiya kwa lengo
la kufanikisha ushindi wa CCM wa mwaka 2020.
Nd.
Mkema alieleza kwamba lengo la ziara hiyo ni kuwakumbusha viongozi na
watendaji wa UWT, majukumu ya msingi yanayotakiwa kufanyiwa kazi kwa
haraka ili kuhakikisha CCM inaendelea kubaki na hadhi yake ya
kusimamisha Dola inayojali misingi ya Demokrasia, Haki na utawala wa
kisheria.
“
Chama Chetu kinajivunia kuwa na jumuiya imara ya Akina Mama ambayo
imekuwa mstari wa mbele kutetea na kupigania maslahi ya CCM bila ya hofu
katika mapambano ya Kisiasa nchini, na kupata ushindi wa kishindo
unaotokana na ridhaa halali ya wananchi”., alisema Mkema na kusisitiza
kuwa Watendaji wa jumuiya hiyo wanatakiwa kutafuta ufumbuzi wa kudumu
juu ya kasoro ndogo ndogo zilizomo katika jumuiya hiyo ili kuongeza
ustawi wa CCM kisiasa nchini.
Alisema
kwamba Akina Mama ndio nyenzo muhimu ya kisiasa kwa chama hicho hivyo
wanatakiwa kuendea na harakati za kujenga ushawishi kwa akina Mama
wenzao waliopo katika makundi na vyama mbali mbali kujiunga na Chama
hicho.
Aliwasihi
Akina Mama hao kuhakikisha afisi za jumuiya hiyo kuanzia ngazi za
Matawi hadi Taifa zinafanya kazi kwa mujibu wa Katiba ya jumuiya na
miongozo ya CCM ili kuongeza kasi za kiutendaji.
Katibu
huyo aliwambia Akina Mama hao kwamba pamoja na kufanya kazi za
kisiasa wanatakiwa kuwa mfano wa kuingwa katika kufanya tafti mbali
mbali juu ya mifumo ya uendeshaji wa Sekta za Afya, Elimu, Miundombinu
na Kilimo kwa lengo la kubaini changamoto zilizomo katika sekta hizo ili
kuishauri serikali kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa sekta hizo.
Aliwashauri
Jumuiya hiyo kuwakumbusha Wanawake wenzao kuhakikisha wanawapa malezi
bora na kufuatilia kwa karibu tabia za watoto wao katika familia ili
waweze kukuwa wakiwa katika maadili mema watakaoweza kushika nyadhifa za
chama na serikali kwa uadilifu hapo baadae.
Alisisitiza
Ushiriki wa Wanawake katika harakati mbali mbali sio tu nafasi za
kisiasa bali waelekeze nguvu na ushawishi wa maendeleo katika Vikundi
vya Ujasiria Mali na Saccos kwa nia ya kupata fursa ya kujiajiri wenyewe
ili waondokane na dhana ya kuwa tegemezi kwa Wanaume.
Mapema
Akimkaribisha Mgeni rasmi, Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo
anayefanyia kazi zake Zanzibar, Bi. Tunu Juma Kondo aliipongeza CCM kwa
kufanya ziara Maalum ya kukutana na watendaji na viongozi hao kwa lengo
la kubadilishana mawazo yatakayosaidia kujenga ufanisi ndani ya chama.
Wakati
huo huo Katibu Mkema , alitembelea Vikundi Vitano (5) vya Ujasiria
Mali vya Akina Mama wa UWT katika Majimbo Chumbuni na Jang’ombe na kuona
kazi mbali mbali zikiwemo za mikono na kilimo zinazofanywa na wanawake
hao kwa lengo la kujikomboa na umasikini.
0 comments:
Post a Comment