Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Muungano na Mazingira Mh.
January Makamba amewataka Wananchi wa Zanzibar
kuulinda na kuuheshimu Muungano pamoja na mapinduzi tukufu ya Zanzibar.
Ameyasema hayo alipokua ziarani Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Aliongeza kuwa anaipongeza Serikali ya Mkoa
kwa juhudi wanazozifanya kuhakikisha
wanasimamia usalama kwa raia wote . Akiwasilisha taarifa kwa Mh Waziri, Katibu tawala wa Mkoa
wa Kasazini Pemba Mohamed Ali alitaja changamoto zinazowakabili ni uchakavu wa
jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa hivyo
kuomba Waziri awsaidie.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Muungano na Mazingira Mh.
January Makamba yupo katika ziara mkoani Kaskazini Pemba pamoja na Unguja.
0 comments:
Post a Comment